Rais wa zamani wa Comoro ahukumiwa jela maisha

Ahmed Abdallah Sambi

Muktasari:

Mahakama nchini Comoro imemhukumu kifungo cha maisha jela aliyekuwa Rais wan chi hiyo, Ahmed Abdallah Sambi baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya uhaini.

Mahakama nchini Comoro imemhukumu kifungo cha maisha jela aliyekuwa Rais wan chi hiyo, Ahmed Abdallah Sambi baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya uhaini.


Sambi mwenye umri wa miaka 64 amehukumiwa leo Jumatatu Novemba 28, 2022 baada ya kupatikana na hatia ya kuuza hati za kusafiria kwa watu wasio na uraia wanaoishi katika Ghuba na alikuwa ameshtakiwa kwa ubadhirifu wa mamilioni ya dola.


Sambi (64) ambaye ni mpinzani mkuu wa Rais wa Comoro Azali Assoumani tayari alikuwa amekaa gerezani kwa miaka minne kabla ya kukabiliwa na kesi.


Sambi ambaye alikuwa Rais wan chi hiyo kati ya 2006-2011 alipitisha sheria mwaka 2008 inayoruhusu uuzaji wa hati za kusafiria za taifa hilo la kisiwa cha Afrika Mashariki kwa ada ya juu.


Hata hivyo maamuzi ya hukumu ya kesi hiyo hayawezi kukatiwa rufaa.