Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ruto ateua mawaziri wapya, awarudisha sita

Muktasari:

  • Leo, Julai 19, 2024, Rais Ruto ametangaza mawaziri wake wapya akiwarejesha sita kwenye nafasi zao na kuwateua wapya wanne. Idadi hiyo ni nusu ya mawaziri waliokuwepo kwenye baraza lake la awali lililokuwa na mawaziri 21.

Nairobi. Rais wa Kenya, William Ruto amewateua mawaziri 10 na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) katika awamu ya kwanza ya uteuzi huo, akiwarejesha sita katika baraza lake jipya na wanne wapya.

Julai 11, 2024, Rais Ruto alivunja Baraza la Mawaziri na kumwacha Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje, Musalia Mudavadi ikiwa ni njia ya kuisuka upya Serikali yake kufuatia mfululizo wa maandamano yaliyoongozwa na vijana maarufu Gen-Z.

Pia, alimwondoa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Justin Muturi akieleza kwamba atahusisha wadau wengine wa kisiasa katika shughuli ya kuunda upya Baraza lake la Mawaziri.

Siku chache zilizopita, Rais Ruto alimteua Mudavadi kuwa msimamizi mkuu wa shughuli za kila siku za wizara zote katika kipindi ambacho hakuna mawaziri husika.

Leo, Julai 19, 2024, Rais Ruto ametangaza mawaziri kwa awamu ya kwanza, wakiwa ni nusu ya mawaziri waliokuwepo kwenye baraza lake la awali lililokuwa na mawaziri 21.

Walioteuliwa na wizara zao ni Profesa Kithure Kindiki (Mambo ya Ndani), Dk Debra Barasa (Afya), Alice Wahome (Ardhi, Ujenzi, Nyumba na Maendeleo ya Miji), Julius Ogamba (Elimu), Aden Duale (Ulinzi) na Dk Andrew Karanja (Kilimo na Maendeleo ya Mifugo).

Wengine ambao ni wapya Roselinda Tuiya (Mazingira, Tabianchi na Misitu), Eric Muuga (Maji na Umwagiliaji), Davis Chirchir (Barabara na Usafirishaji), Margaret Ndung’u (Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidigitali).

Vilevile, Rais Ruto amemteua Rebecca Miano kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) akichukua nafasi ya Muturi.

Rais Ruto anaendelea kuunda Baraza la Mawaziri wakati vuguvugu la maandamano nchini humo likiendelea, vijana wa Gen-Z wanashinikiza kiongozi huyo pia aondoke madarakani kwa kuwa serikali yake imeshindwa kupunguza makali ya maisha, huku kodi zikiongezeka.

Wanadai kiongozi huyo wa nchi amewasaliti kwa kutotimiza aliyowaahidi wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2022 na kuwa Serikali yake inatawaliwa na rushwa.

Kumekuwa na taarifa kwamba Rais Ruto amekuwa akikutana na kiongozi wa upinzani, Raila Odinga kwa mashauriano ya kuunda serikali ya mseto ili kutuliza ghasia zinazotokea katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Juzi Raila alitoa kauli ikionye juu ya kumwondoa Ruto madarakani kwamba haitasaidia kitu, kwa kuwa badala yake ataingia naibu wake, Rigathi Gachagua na mambo yatakuwa yaleyale.