Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Thabo Bester na mpenzi wake watua Afrika Kusini chini ya ulinzi mkali

Muktasari:

  • Mfungwa aliyetoroka gerezani nchini Afrika Kusini na kukamatwa hapa nchini jijini Arusha, Thabo Bester amerudishwa nchini kwao Afrika Kusini pamoja na mpenzi wake Nandipha Magudumana tayari kwa ajili ya hatua za kisheria.

Johannesburg. Mhalifu aliyetoroka gerezani nchini Afrika Kusini na kukamatwa hapa nchini mjini Arusha, Thabo Bester pamoja na mpenzi wake Nandipha Magudumana wamerejea nchini Afrika Kusini na ndege maalumu na kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Lanseria mapema leo Alhamisi asubuhi nchini humo.

Wawili hao walinaswa nchini Tanzania Ijumaa iliyopita baada ya kutoroka kwa katika kituo cha kurekebisha tabia cha Mangaung Mei mwaka jana.

Gari la polisi lilionekana likitoka kwenye ndege, ambayo ilitua majira wa saa nne asubuhi nchini humo.

Mkutano wa wanahabari umepangwa kufanyika nchini humo ambapo Waziri wa Sheria Ronald Lamola na waziri wa polisi nchini humo, Bheki Cele, wanatarajiwa kutoa maelezo zaidi.

Ujumbe wa kuwarejesha watuhumiwa hao wa uhalifu kutoka Afrika Kusini uliwasilishwa Tanzania ili kupata uhamisho wa kurejea nchini humo ambao umekamilika leo.

Bester, ni mhalifu maarufu kutoka Afrika Kusini anayejulikana kama ‘Muuaji wa Facebook’. Bester mwenye umri wa miaka 46 alipata umaarufu kufuatia namna alivyokua akiwarubuni wanawake kupitia mtandao wa Facebook ambapo mwaka 2012 mahakama nchini humo ilimtia hatiani kwa kosa la kuwarubuni wanawake wawili na kuwabaka na kumuua mmoja.

Bester ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha maisha jela kufuatia kosa hilo mauaji, alitoroka katika Kituo cha cha Mangaung huko Bloemfontein Mei 2022 baada ya awali kuaminika kuwa alijiua kwa kujichoma moto.

Thabo Bester na Dk Nandipha Magudumana kwa pamoja wanakabiliwa na makosa ya utapeli baada ya kutengeneza kampuni feki ya ujenzi na kufanikiwa  kuwatapeli watu wengi mamilioni ya Randi.

Bester yeye anakabiliwa na kosa la kutoroka gerezani alikokua akitumikia kifungo cha maisha huku Dk Nandipa akihumiwa katika makosa ya kufanya mpango wa kutoroka kwa Bester lakini pia kumficha Bester baada ya kufanikiwa kutoroka gerezani.