Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VIDEO: Muuaji wa Afrika Kusini aliyetoroka gerezani akamatwa Arusha

Muktasari:

  • Raia wa Afrika Kusini, Thabo Bester aliyetoroka gerezani nchini humo, amekamatwa nchini Tanzania akiwa na wenzake wawili.

Johannesburg/Dar. Mhalifu wa makosa ya mauaji na ubakaji kutoka Afrika Kusini, Thabo Bester amekamatwa jijini Arusha nchini baada ya kusakwa kwa muda mrefu.

 Taarifa iliyotolewa leo Aprili 8 na Jeshi la Polisi Tanzania katika ukurasa wake wa Instagram imesema Bester amekamatwa akiwa na wenzake wawili wakiwa jijini Arusha.

“Ni kweli makachero wetu wamewakamata Thabo Bester, Dk Nandira Magudumana na Zakaria Alberto na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.

“Taratibu za mawasiliano ya kisheria ya ndani nay a kimataifa zinaendelea kukamilishwa,” imesema taarifa hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Pretoria leo kupitia mtandao wa APANews, Waziri wa Sheria wa Afrika Kusini, Ronald Lamola amesema, Bester alinaswa jijini Arusha Tanzania Ijumaa usiku pamoja na mpenzi wake wa Afrika Kusini Nandipha Magudumana na mtu mwingine kutoka Msumbiji.

"Tunaweza kuthibitisha kwamba Thabo Bester na msaidizi wake Magudumana wamekamatwa nchini Tanzania," Lamola amesema.

Kwa upande wa Waziri wa Polisi wa nchi hiyo, Bheki Cele alisema kukamatwa kwa Bester kuliwezekana kupitia ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi la Afrika Kusini, Jeshi la Polisi la kimataifa (Interpol) na polisi wa Tanzania.

Mfahamu muuaji wa Afrika Kusini aliyetoroka gerezani, kukamatwa Arusha

"Walionekana wakitoka Dar es Salaam na kufuatwa hadi walipofika Arusha. Ilibainika kuwa walikuwa na hati za kusafiria kadhaa na hakuna hata moja kati ya hizo ambayo imegongwa muhuri nchini Afrika Kusini na Tanzania," Cele amesema.

Wawili hao wamekuwa wakijificha tangu Bester alipobainika kutoroka gerezani nchini humo.

Bester, ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha maisha jela kwa mauaji, alitoroka katika Kituo cha cha Mangaung huko Bloemfontein mnamo Mei 2022 baada ya awali kuaminika kuwa alijiua kwa kujichoma moto.

Hata hivyo, Idara ya Huduma za Urekebishaji ya nchi hiyo ambayo awali ilitangaza kuwa amefariki, ilithibitisha kuwa mwili uliochomwa moto uliopatikana katika chumba alichokua Bester haukuwa wa muuaji na mbakaji huyo.

Bester, anayejulikana kama 'mbakaji wa Facebook', alipatikana na hatia mwaka 2012 kwa kuwabaka wanawake wawili na kumuua mmoja, baada ya kuwarubuni kwa kutumia mtandao wa Facebook.

Mnamo Machi mwaka jana maafisa waliripoti kwamba alikufa katika moto katika Kituo cha Mangaung, karibu na Bloemfontein.

Hata hivyo, hivyo baadaye ilionekana Bester alitoroka wakati wa moto na amekuwa akiishi maisha ya kifahari katika kitongoji cha kifahari cha Hyde Park mjini Johannesburg.

Kwa mujibu wa taarifa zilizofichuliwa kwa mara ya kwanza na kituo cha habari cha Afrika Kusini cha GroundUp na kuthibitishwa na polisi, maiti iliyokutwa imechomwa haikuwa ya Bester, kutokana na uchunguzi wa DNA uliothibitisha.

Matokeo ya uchunguzi wa maiti yamebaini kuwa mtu aliyepatikana amekufa kwenye chumba alichokuwa Bester kifo hicho kilisababishwa na kuweweseka kabla ya moto.

Moto huo unaonekana kuwa sehemu ya tukio la kutoroka jela la Bester ambalo limezua maswali mengi kuhusu uwezekano wa kuhusika kwa maafisa wa magereza.

Lakini mwisho wa wiki iliyopita, polisi walisema vipimo vya DNA vilivyopatikana katika gereza alilokuwemo vilibainisha kuwa vya mtu mwingine. 

“Katika hali hii, kipaumbele chetu ni kujua aliyekimbia mkono wa haki nan a kujua jinsi alivyoghushi kifo," amesema msemaji wa Polisi Athlenda Mathe aliposhughumza na shirika la habari la AFP Jumatatu iliyopita.

Kesi hiyo imevuma mno nchini Afrika Kusini, ambako makundi ya haki za wanawake yamekuwa yakiilaumu Serikali kwa kushindwa kuwalinda dhidi ya ukatili. 

“Kisa hiki kimekuwa kama filamu na kimetikisa kila mtu… nashindwa kuamini alivyovyoweza kuwafanyia waathirika,” amesema Bafana Khumalo ambaye ni mkurugenzi mwenza wa shirika Sonke Gender Justice.

Kati ya Oktoba na Desemba mwaka uliopita polisi waliripoti matukio 12,000 ya ubakaji nchini humo.

Picha zinazodhaniwa kuwa za mhalifu huyo zikimwosnyesha akiwa yuko katika duka maarufu jijini Johannesburg zilionyeshwa.

Pia baadhi ya wanawake wamedai kuwasiliana naye kupitia mitandao ya jamii.

Pamoja na kutoroka, Bester pia alidaiwa kuendesha bishara ya habari ya kitapeli akiwa gerezani na kuna video ya mhalifu akitoa maelezo kwenye tukio la kampuni kwa njia ya video akijifanya yuko New York nayo imevuma.


Nyongeza kwa msaada wa mitandao.