Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Uchaguzi DRC waiva, CENI yapokea vifaa

Picha na UN News

Muktasari:

  • Maandalizi uchaguzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) yashika kasi huku Tume ya Uchaguzi (CENI) ikithitibisha kupokea vifaa kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika Desemba 20, mwaka huu.

Dar es Salaam. Zikiwa zimesalia siku tisa kabla ya uchaguzi wa DRC ufanyike, Tume Huru ya Uchaguzi (CENI) imethibitisha kupokea vifaa vyote kutoka nchini China kwaajili ya zoezi hilo.

Kupitia tovuti ya DW tume hiyo imepokea zaidi ya kilo 92,000 za vifaa vya uchaguzi mwishoni mwa wiki ambavyo ni mzigo wa mwisho unaojumuisha hati nyeti,karatasi za matokeo na za maelezo kuhusu uchaguzi.

Akinukuliwa na DW mmoja wa wasemaji wa CENI, Jean-Claude Munganga, amesema kuwa Desemba 20 kutakuwa na uchaguzi kwa sababu vifaa vyote vipo tayari na vimesambazwa.

“Vifaa hivyo ni karatasi za matokeo, wino usiofutika, karatasi za maelezo, vyeti vya kura na vifaa vingine. Kimsingi kila kitu kiko tayari na tunachosubiri ni siku ya uchaguzi tu," amesema Munganga.

Wakati CENI ikitoa hakikisho hilo, wagombea wa kinyang’anyiro cha urais wameendelea na kampeni maeneo mbalimbali nchini humo akiwemo Felix Tshisekedi anayetetea kiti chake.

Wagombea wa upinzani wakiwemo Martin Fayulu, aliyekuwa Gavana wa Katanga Moise Katumbi na daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama aliyeshinda Tuzo ya Nobel, Dennis Mukwege, wote wamefanya kampeni mashariki mwa nchi hiyo wakiahidi utulivu kutokana na ghasia zilizopo.

Mchuano mkali unatarajiwa kuwa kati ya Rais Tshisekedi, Fayulu, Mukwege na Fayulu ambaye katika uchaguzi wa mwaka 2018 ilipewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi lakini matokeo yalipotakangwa hakufua dafu.