Upekuzi wa polisi wabaini mwandishi kuuawa ubalozini

Muktasari:

  • Kutokana na ushahidi huo, mamlaka za Uturuki zilionekana kuwa zimejiandaa kufanya upekuzi katika makazi jirani ya balozi mdogo baada ya mwanadiplomasia huyo kuondoka nchini.
  • Maoni ya ofisa wa Uturuki aliyotoa kwenye shirika la The Associated Press yamezidisha mbinyo dhidi ya Saudi Arabia ikitakiwa kueleza nini kilimtokea Khashoggi, aliyetoweka Oktoba 2 alipotembelea ubalozi huo mdogo kwa ajili ya kupatiwa nyaraka zilizohitajika ili aweze kuoa.


Istanbul, Uturuki. Polisi waliokuwa wanafanya upekuzi katika mejengo ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia uliopo mjini Istanbul umepata ushahidi kwamba mwandishi wa habari Jamal Jamal Khashoggi aliuawa ndani, ofisa wa ngazi ya juu wa Uturuki alisema Jumanne.
Kutokana na ushahidi huo, mamlaka za Uturuki zilionekana kuwa zimejiandaa kufanya upekuzi katika makazi jirani ya balozi mdogo baada ya mwanadiplomasia huyo kuondoka nchini.
Maoni ya ofisa wa Uturuki aliyotoa kwenye shirika la The Associated Press yamezidisha mbinyo dhidi ya Saudi Arabia ikitakiwa kueleza nini kilimtokea Khashoggi, aliyetoweka Oktoba 2 alipotembelea ubalozi huo mdogo kwa ajili ya kupatiwa nyaraka zilizohitajika ili aweze kuoa.
Hivi karibuni Rais Donald Trump wa Marekani alitoa kauli iliyoonekana kutetea akisema: “Mwana mfalme alinieleza kwamba tayari ameshaanza, na atapanua kwa haraka upekuzi kamili na kamilifu juu ya suala hili. Majibu yatapatikana hivi karibuni."
Trump baadaye alionekana kuchukua msimamo mkali kuitetea Saudi Arabia akikosoa shutuma zinazotolewa na jumuiya ya kimataifa dhidi ya Ufalme na akafananisha na shutuma za shambulio la kingono alizotupiwa Jaji wa sasa wa Mahakama ya Juu Brett Kavanaugh wakati wa mchakato wa kuthibitishwa kwake.
"Hapa tumerudi tena kwamba unakuwa mkosaji hadi ithibitishwe kwamba huna hatia,” Trump alisema katika mahojiano na AP