Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waangalizi wa EAC kutoshiriki uchaguzi DRC

Kinshasa. Waangalizi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) huenda wasishiriki katika uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) unaotarajiwa kufanyika Desemba 20, mwaka huu.

Rais wa Tume Huru ya Uchaguzi ya DRC (CENI), Denis Kadima amelithibitishia Mwananchi Jumamosi iliyopita kwamba hadi sasa wawakilishi kutoka EAC hawakuwa miongoni mwa waangalizi wa kimataifa ambao wameidhinishwa na CENI.

"Hadi sasa hatujapokea ombi lolote kwa hivyo hatujaidhinisha mtu yeyote kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki," alisema Kadima wakati wa mahojiano na maalum na waandishi wa habari kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambao wako nchini humo kwa ajili ya kuripoti uchaguzi.

Aliongeza: “Kwa kawaida, waangalizi wa kimataifa hutuma maombi yao Wizara ya Mambo ya Nje. Baada ya kuthibitishwa, tunaarifiwa na tunatoa kibali. Sijui EAC iliwahi kuomba kibali kutoka wizarani au la. Nadhani wizara itakuwa katika nafasi nzuri ya kujibu hilo.”

Kundi lingine maarufu la waangalizi ambao watakosa fursa ya kuangalia uchaguzi ni wale kutoka Umoja wa Ulaya (EU). Kwa mujibu wa Kadima, kibali cha waangalizi wa Umoja wa Ulaya kiliondolewa na serikali baada ya kundi hilo kuomba kuleta vifaa vya mawasiliano ambavyo serikali haikuidhinisha.

"Hapo awali tuliidhinisha waangalizi kutoka EU. Lakini baadaye waliiambia serikali kuwa wanataka kuleta vifaa vya mawasiliano ambavyo haviendani na masharti yaliyowekwa na serikali, hivyo kibali chao kiliondolewa,” alifafanua Kadima na kuongeza kuwa hadi kufikia sasa EU imeondoa sehemu kubwa ya waangalizi wake.

"Kuna waangalizi wachache kutoka EU ambao bado wako nchini lakini wigo wao wa kazi hautajumuisha kile walichopanga kufanya kama vile kukusanya matokeo ya uchaguzi kutoka vituo vya kupigia kura. Hawawezi kufanya hivyo kwa sababu vifaa walivyopanga kutumia kufanya hivyo vimekataliwa na serikali,” alisema.

Wakati huohuo, wakati waangalizi wa EAC wakikosekana, wenzao wa SADC wameshaanza kazi. Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC (SEOM) chini ya uongozi wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Zambia, Enoch Kavindele ambaye alisema wakati wa uzinduzi Jumamosi kuwa timu hiyo iko DRC tangu Desemba 6, mwaka huu.

"Katika kipindi hiki tumebaini kuwa uchaguzi wa Rais, Wabunge na Majimboni  uliopangwa kufanyika Desemba 20, 2023 unatawaliwa na Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na sheria husika," alisema.