Waziri wa Uingereza ajiuzulu, kisa Rwanda

Uingereza. Waziri wa Uhamiaji nchini Uingereza, Robert Jenrick amejiuzulu jana Jumatano kwa madai sheria ya dharura ya Serikali ya Rwanda kuwa haijitoshelezi.

Katika barua yake ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak, waziri huyo amesema waziri mkuu ameelekea kwenye msimamo wake kuhusu kutokubaliana na sheria hiyo ya dharura.

"Hata hivyo, sikubaliani na sheria inayopendekezwa kwa sasa kupitia Bunge, kwani siamini kwamba inatupa fursa nzuri zaidi ya kufanikiwa," amesema Jenrick.

Amesema umakini zaidi ulihitajika kumaliza changamoto za kisheria ambazo zinaweza kukwamisha mpango huo wa Serikali ya Uingereza na Rwanda.

Muswada huo uliozinduliwa hivi karibuni na umeweka wazi kwamba Rwanda kuwa ni nchi salama kwa wanaotafuta hifadhi.

Hata hivyo, waziri mkuu ameelezea kujiuzulu Jenrick kama ni jambo la kuvunja moyo na kutokana na kutoelewa mkataba huo.

Mkataba huo unawahakikisha watu waliohamishwa hadi Rwanda hawako katika hatari ya kurejeshwa katika nchi ambayo maisha au uhuru wao utatishiwa.

Mpango wa Rwanda ni sehemu ya mkakati wa kupunguza idadi ya watu wanaoingia Uingereza kwa kuvuka bahari kwa boti.