Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wenye ajira, vijana kuathiriwa na sheria mpya ya kodi

 Rais wa Kenya, William Rutto.

Muktasari:

  • Katika Mswada wa Fedha wa 2023, ambao umeabeba mapendekezo ya utozaji kodi kwa mwaka wa kifedha wa 2023/24, Hazina inapanga hatua kadhaa ambazo zitawaacha watu wa tabaka la kati, ambao kimsingi ndiyo wamekuwa wakibanwa na serikali katika mkakati wake wa kuongeza mapato.

Nairobi. Vijana wabunifu wa maudhui ya kidijitali na watu wa kipato cha kati, ni miongoni mwa wakenya watakao athiriwa kimapato ikiwa Bunge la nchi hiyo litaidhinisha mpango wa kutanua wigo wa kodi uliopendekezwa na serikali ya Rais William Ruto.

Katika Mswada wa Fedha wa 2023, ambao umeabeba mapendekezo ya utozaji kodi kwa mwaka wa kifedha wa 2023/24, Hazina inapanga hatua kadhaa ambazo zitawaacha watu wa tabaka la kati, ambao kimsingi ndiyo wamekuwa wakibanwa na serikali katika mkakati wake wa kuongeza mapato.

Muswada huo umependekeza kukatwa kwa asilimia 3 kutoka ya mishahara (basic salary) ambayo itaelekezwa kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Makazi wa Taifa, ambapo mwajiri pia atatoa mchango sawa na ule wa mfanyakazi.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Nation la Kenya, Wakenya wanaopata angalau Sh500,000 za kenya kila mwezi, wanakabiliwa na ongezeko kubwa la kodi, kwani muswada unapendekeza kuongeza ushuru wao kutoka asilimia 30 hadi asilimia 35.

Hii inamaanisha, mfanyakazi anayepokea Sh500,000 kwa mwezi, atalazimika kulipa Sh200,000 kama kodi ya mapato. Pendekezo hilo linajiri wakati ambapo Rais Ruto amekuwa msimamo kwa matajiri, huku akipendekeza kuanzishwa kwa ushuru wa ukwasi.

Hata hivyo, inasemekana kuwa maumivu hayatawapata wenye ajira pekee, kwani Hazina pia inapendekeza kuwatoza kodi waandaji wa maudhui ya kidijitali, tasnia ambayo imewavutia vijana, ikitoa njia mbadala kwa jamii iliyoathiriwa sana na ukosefu wa ajira.

Mswada huo unapendekeza ushuru wa asilimia 15 kama kodi ya zuio, kwa malipo yanayotokana na maudhui ya kidijitali.

Wachambuzi wansema ushuru huo utakuwa na athari kubwa kwa maelfu ya vijana ambao kwa sasa wanapata riziki zao kutokana na tasnia hiyo, na mpango huo unakuja kipindi ambacho serikali ikiwekeza zaidi katika mawasiliano ya intaneti na teknolojia ili kuvutia wasio na ajira.

Kwa upande mwingine, Hazina pia imependekeza kuongeza ushuru kutoka asilimia 1 hadi 3 kwenye biashara zenye mapato kuanzia Sh500,000 lakini hayazidi Sh15 milioni, hatua ambayo itaathiri biashara nyingi ndogo na za kati (SMEs) na hivyo kusifanya zisiwe na uhimilivu.

Serikali pia inapendekeza kutoza kodi kwenye bidhaa mbalimbali ambazo ni pamoja na samaki kutoka nje (Sh100,000 kwa tani moja au asilimia 20 ya thamani) na juisi ya unga (Sh25 kwa kilo).

Wale wanaotumia bidhaa za urembo kama vile mawigi, ndevu, nyusi na kope, na kucha za bandia, watatozwa ushuru wa asilimia 5, huku serikali ikiweka bidii kwenye tasnia ya urembo hiyo ambayo katika muongo mmoja uliopita imekua kwa kiasi kikubwa.

Waagizaji saruji watalipa ushuru wa asilimia 10 kwa kilo moja ya bidhaa, au Sh1.50 kwa kilo, kutegemea ni ipi iliyo juu zaidi.