Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

70 wajeruhiwa ajali ya treni ya TRC

Muktasari:

  • Treni ilikuwa na abiria 571, ajali imetokea baada ya mabehewa sita kuacha njia

Dar es Salaam. Treni ya abiria ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) iliyokuwa ikitokea mkoani Kigoma kuelekea mikoa ya Tabora, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam imepata ajali.

Watu 70 wamejeruhiwa katika ajali hiyo kati ya 571 waliokuwa wakisafiri kwa treni hiyo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TRC, Jamila Mbarouk katika taarifa kwa umma leo Agosti 28, 2024 amesema treni hiyo namba Y14 ikiwa na kichwa namba 9002, mabehewa 12 ya abiria, behewa moja la vifurushi (parcel) na behewa moja la breki imepata ajali kati ya Stesheni ya Kazuramimba na Uvinza mkoani Kigoma saa 7.30 usiku wa Agosti 28, 2024.

“Ajali imetokea baada ya mabehewa sita ya treni kuacha njia na kusababisha majeruhi 70, wanawake 26 na wanaume 44. Treni ilikuwa na jumla ya abiria 571 wakisafiri kutoka Kigoma kuelekea mikoa ya Tabora, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam,” imeeleza taarifa hiyo.

TRC imesema kwa kushirikiana na Kitengo cha Afya cha Mkoa wa Kigoma waliwapeleka majeruhi katika Hospitali ya Wilaya ya Uvinza kwa matibabu.

Amesema hali za afya za majeruhi zinaendelea kuimarika na kwamba, 57 wameruhusiwa.

TRC imesema majeruhi wanane wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Uvinza na watano wamehamishiwa Hospitali ya Maweni.

“Treni iliendelea na safari kuelekea mikoa ya Tabora, Dodoma, Morogoro, Pwani na Dar es Salaam. Shirika linawapa pole majeruhi na linaendelea na jitihada za kuwahudumia. Hakuna taarifa ya vifo vilivyotokana na ajali,” limeeleza TRC.