‘Mila zimemjenga mwanaume kuwa siongozwi na mwanamke’

Muktasari:

  • Suala la usawa kuonekana mashindano yenye lengo la kuchukua nafasi ya mwanaume kwenye jamii, limetajwa kuwa sababu ya kutopatikana kwa sawa wa uongozi kwenye jamii.

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (Tamwa), Rose Reuben amesema kinachosababisha kutofikiwa usawa wa kijinsia ni kutokana na agenda hiyo kuonekana ni mashindano ya kutaka kuchukua nafasi ya mwanaume.

Amesema mazingira bora yakiwekwa ya mwanamke kuwa kuowa kiongozi hawezi kurudi nyuma.

Hayo ameyazungumza leo Machi 8, 2023 katika mjadala unaoendeshwa na Mwananchi kupitia mtandao wa Twitter, Mwananchi Twitter space ukijadili ‘Nini kifanyike kuwepo kwa usawa katika nafasi za Uongozi Tanzania.

Rose amesema dhana ya mwanamke kuwa kiongozi kuchukuliw akama mashindano kumechangia kunawekwa vigingi ya wanawake kutochukua nafasi ya mwanaume.

“Kuna vitu kama mila na desturi na tamaduni zilizomjenga binadamu katika mazingira yake ambapo hili la mila zimemjenga mwanaume kuwa siongozwi na mwanamke,”amesema.

Kutokana na dhana hiyo Rose amesema mwanamke anaposhika nafasi ya uongozi jamii imekuwa ikimtafsiri kama nafasi hiyo ni ya kupewa hivyo si kiongozi halali.

Ili kuondoa tabia hiyo, amesema ni muhimu kubadili mtazamo kwani sharia zinaweza kuwepo lakini kama mitizamo haitabadilikabado nafasi ya mwanamke kuongoza itakuwa finyu.

“Ningependa kuinona Tanzania ambayo itawaoa wanake kama viongzi halali, hata kama sheria hazijawekwa wamtii ambaye ni kiongozi bila tatizo lolote,”amesema.

Amesema ni muhimu wanawake wapewe nafasi ya uongozi kulingana na uwezo waliouonyesha akisistiza pia yapo mazingira ya kazi ambayo yanapaswa kuondolewa aliyoyataja kudhoofisha juhudi za wanawake kama rushwa ya ngono au unyanyasaji wa kingono.

“Tulifanya utafiti kwanini vyombo vya habari havitangazi habari za jinsia tukagundua tatizo la rushwa ya ngono ni kubwa pia tukagundua waandishi hawakumbuki kuandika habari zao hata kama hawajalipwa mishahara miaka mitano ni rahisi kuandika habari za taasisi zingine kwamba hawajapata mishahara,”amebainisha.

Naye Paul James amesema ni muimu wanawake kusimama kwa  pamoja kutafuta sheria zinazowasimamia ili kupinga ukandamizaji wanaoupitia.