Radi yaua watoto wanne Kigoma

Wednesday January 05 2022
Radi pc
By Happiness Tesha

Kigoma. Watu watano wakiwemo  watoto wanne wa familia tofauti wamepoteza maisha baada ya kupigwa na radi wakiwa wanacheza chini ya mti wakati mvua ikiwa inanyesha.

Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma, James Manyama amesema tukio hilo limetokea Januari 4, 2022, majira ya saa 12 jioni, katika kijiji cha Kibuye kata ya Kumsenga , wilayani Kibondo.

Amesema watoto hao wanne ni wa familia moja tofauti na mtu mzima mmoja aliyefahamika kwa jina la Annatoria Muhoza (50), aliyepigwa na radi wakati akiwa shambani analima.

Kamanda Manyama amewataka wazazi na wananchi wa mkoa wa Kigoma kuchukua tahadhari kipindi hiki cha mvua ikiwamo kudhibiti watoto kucheza chini ya miti.

Advertisement