: RC atoa maagizo kamati ya usalama Kahama

Muktasari:
- Nendeni mkampe ushirikiano DC mpya Mkinda kama mliokuwa mkinipatia mimi, mkasikilize kero za wananchi na kutatua migogoro.
Shinyanga. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mboni Mhita ametoa maagizo kwa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama, kutoa ushirikiano kwa Mkuu mpya wa Wilaya ya Kahama, Frank Mkinda kama waliokuwa wakimpa pamoja na kusikiliza kero za wananchi.
Akizungumza leo Julai 01, 2025 katika hafla fupi ya uapisho wa Mkinda iliyofanyika ofisini kwake.
Kwa upande wake Mkinda amesema kuwa yuko tayari kupokea maagizo yoyote atakayopewa katika kuijenga Kahama na mkoa kwa ujumla,
“Kwa sababu leo ni siku ya kwanza na Kahama sijawahi kufika niombe ridhaa ya mkuu wa mkoa kusikiliza kile atakachoniagiza kwenda kufanya kwa ajili ya Kahama na kukitekeleza” amesema Mkinda.
Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro amesema kuwa watashirikiana kwa pamoja na kusaidiana kama kuna kitu mmoja atakwama katika kutekeleza wajibu wao.
“Tulikuwa na dada yetu Mhita na sasa tumeletewa mdogo wetu Frank ambaye tutamuonyesha ushirikiano na kwa pamoja tutasikiliza kero na kutatua changamoto za wananchi” amesema Mtatiro.