Ukarabati wa hospitali ya wilaya Kiteto kugharimu Sh900 milioni

Naibu Waziri wa Tamisemi, Dk Festo Dugange akizungumza na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Kiteto baada ya kukagua ujenzi wa Sh900 milioni unaofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto. Picha na Mohamed Hamad

Muktasari:

  • Naibu Waziri Tamisemi, Dk Festo Dugange afurahishwa na maamuzi ya utekelezajo wa mradi huo kwa fedha hizo

Manyara. Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto, John Nchimbi amemweleza Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Dk Festal Dugange kuwa majengo yaliyopo katika hospitali ya wilaya hiyo kwa sasa hayana hadhi.

Kutokana na hilo amesema hatua ya Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassani kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati huo kitasaidia wananchi hao kuondokana na adha ya kupata huduma.

"Majengo yaliyopo sasa ni ya miaka 70, hivyo hayatoshi kwa wakati huu lakini kwa sasa yasingeliweza pia kutosha tena, tumepata fedha za majengo matatu, mahitaji ni saba, tuna Sh900 milioni bado tunauhitaji mkubwa sana wa majengo zaidi kukidhi haja ya hospitali ya wilaya," amesema Nchimbi.

Kwa upande wake Ofisa Tawala mkoa wa Manyara, Caroline Mthapula amesema halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ni miongoni mwa zinazofanya vizuri katika miradi ya wananchi.

 "Halmashauri ya Kiteto ni miongoni mwa halmashauri za mkoa wa Manyara zinazofanya vizuri, ukileta fedha hapa huna wasiwasi hata ufuatiliaji wake unakuwa mdogo sana na ukija huku unaona kitu chenye ubora na kinaisha kwa wakati" amesema.

Akizungumzia usimamizi wa majengo hayo Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mbaraka Batenga, amesema katika ukaguzi anaofanya yeye huelekeza mafundi hao mbali na kipimo wanachotumia cha kitaalam kuwasaidia pia wawe na jicho lingine katika ujenzi huo.

"Nikija hapa panachimbika huwa nasimamia tufali linavyolala unajengaje yaani nawaambia hawa wakati unajenga mbali na kipimo uwe na pimamaji ya jicho na huwa na sema kwa umri huu kama mimi sijui ujenzi najua nini sada" amesema DC Batenga

Kwa upande wake Dk Ndugage ameeleza kufurahishwa kwake na mpango huo ambao unaonyesha baada ya miezi mitatu majengo hayo yatakamilika.

"Fedha zimekuja nimefurahi sana na mpango kazi mliojiwekea kuhakikisha mnakwenda kukamilisha majengo haya matatu ndani ya miezi mitatu mliojiwekea wenyewe ifikapo june akinamama wajawazito, jengo la upasuaji yote haya yatakuwa yamekamilima.