UVCCM waomba kusimamia sensa

Muktasari:

  •  Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro wameiomba Serikali kuwapa nafasi ya kusimamia sensa pindi itakapoanza.

  


Rombo. Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro wameiomba Serikali kuwapa nafasi ya kusimamia sensa pindi itakapoanza.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa UVCCM Rombo, John Kanyau wakati wa mkutano wa chama hicho uliofanyika wilayani humo.

"Tunaiomba Serikali nafasi ya ajira inapotokea iwakumbuke vijana ambao wamekuwa wakijitolea tunajua sensa itafanyika hivi karibuni kwa hiyo inapotokea fursa kama hiyo Serikali iwakumbuke vijana hawa.

"Tunaomba vijana hawa waingie moja kwa moja kusaidia hii shughuli nzima ya sensa kwa sababu ni maeneo yao ya kujidai na na ndio wenye ilani ya chama cha Mapinduzi," amesema

Naye mbunge wa Rombo ambaye pia ni Waziri wa kilimo nchini, Profesa Adolf Mkenda amewaondoa hofu vijana hao kuhusu ajira huku akisema Serikali ina mpango wa kuajiri vijana wengi zaidi huku akiwataka panapotokea fursa ya ajira kuwa mstari wa mbele.