Wananchi wajenga kituo cha polisi
Muktasari:
Wananchi waliohojiwa walisema kwamba wanaamini kuwa ujenzi wa kituo hicho utakuwa sababu ya kupunguza uhalifu katika maeneo yao.
Kilombero. Kutokana na uhalifu uliokithiri Kata ya Namwawala wilayani Kilombero, wananchi wameamua kujenga kituo cha polisi kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama.
Akizungumza na wananchi wake kwenye mkutano wa kujadili maendeleo, Diwani wa Kata ya Namwawala, Godfery Lwena amesema ujenzi huo utaanza Septemba mwaka huu katika eneo la Boma Mjinga.
Amesema ujenzi wa kituo hicho utapunguza ama kumaliza kabisa vitendo vya uhalifu vinavyofanyika katika Kijiji cha Namwawala, Idandu na Kisegese.
“Wananchi wamekuwa wakitaabika kwa kukosa kituo cha polisi karibu pindi kunapotokea vitendo vya uhalifu katika kijiji,” amesema Kombo.
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kisegese, Juma Shaaban na Hamisa Abdallah, wamesema kuwa ujenzi wa kituo hicho utakapokamilika utasaidia kupunguza uhalifu.