Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Afariki dunia akivua samaki

Muktasari:

Ni katika ziwa Victoria jijini Mwanza

 


Buchosa. Leonard Emmanuel (35)  mkazi wa kijiji cha Luhama mkoani Mwanza amefariki dunia baada ya kuzama katika ziwa Victoria wakati akivua samaki.

Tukio hilo limetokea leo Ijumaa Julai 13, 2018 katika kijiji hicho kilichopo Kata ya Bangwe Halmashauri ya Buchosa Wilaya ya Sengerema, ikielezwa kuwa marehemu alikuwa akivua samaki kwa kutumia ndoano huku akiwa katika maboya, badala ya mtumbwi.

Ofisa mtendaji wa Kata ya Bangwe,  Benard Bwaila amesema baada ya kupata taarifa alifika eneo la tukio  na kuanza kumtafuta marehemu na kukuta mwili wake ukielea.

Kufuatia tukio hilo, Bwaila amepiga marufuku watu kutumia vyombo vya uvuvi visivyo rasmi kwa maelezo kuwa wanahatarisha maisha yao.

Baba mkubwa wa marehemu, Yohana Masome ameieleza MCL Digital kuwa Emmanuel alikuwa na wenzake wakivua samaki lakini baada ya kuona upepo umekuwa mkali, waliamua kuondoka lakini marehemu alibaki na kuwaeleza kuwa anatafuta kitoweo cha watoto wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema hana taarifa za tukio hilo, kubainisha kuwa atatoa ufafanuzi atakapopata taarifa.