Ahadi ya mrithi wa Dk Munga

Friday November 27 2020
mrithipic
By Mwandishi Wetu

Lushoto. Askofu mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dk Msafiri Mbilu ameahidi kurejesha umoja na mshikamano ili kuleta maendeleo ya kanisa hilo.

Amesema atahakikisha misingi ya kanisa hilo anaisimamia kikamilifu katika kuwajenga kiimani waumini na kuimarisha mahusiano.

Ahadi hiyo ameitoa mara baada ya kutangazwa mshindi  baada ya kupata kura 197 za wajumbe wa mkutano mkuu wa Dayosisi hiyo kati ya kura 217 zilizopigwa. Kura 11 zikiharibika na 12 zilikuwa za hapana.

Dk Mbilu anakuwa mrithi wa Askofu mstaafu wa Dayosisi hiyo, Dk  Stephen Munga.


Advertisement