Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ahamasisha kilimo cha mbogamboga kuimarisha lishe

Muktasari:

Mkazi wa Mbozi mkoani Songwe ameanzisha kilimo cha bustani nyumbani kwake huku akihamasisha wanajamii kulima kilimo hicho ili kuhamasisha upatikanaji wa chakula na kuimarisha lishe.

Songwe. Mkazi wa Ichenjezya katika halmashauri ya Mbozi mkoani hapa, Allen Seme (67) ameanzisha bustani za vichuguu na kupanda mbogamboga na matunda katika eneo dogo la makazi yake kwa ajili ya kujipatia lishe na kipato.

Akizungumza leo Oktoba 18 na mwandishi wa habari hizi ambaye amejionea jinsi anavyolima kilimo cha vichuguu kwa lengo la kujikwamua kimaisha na kupata lishe huku ziada akiwauzia majirani zake.

Seme amesema ameamua kulima kilimo cha vichuguu baada ya kuona matunda na mbogamboga ni muhimu katika kulinda mwili na kusaidia kuondoa udumavu wa akili katika jamii zetu.

"Mwaka 1996 niliipata ugonjwa wa kisukari ambapo nilihangaika katika hospitali mbalimbali baadaye nilikumbuka kuwa hakuna tiba ya ugonjwa huo, ndipo nilipoamua kutumia elimu yangu kuboresha lishe, huu ndiyo ulikuwa mwanzo wa kilimo hiki Ili nijipatie lishe yangu," amesema Seme.

Pia amesema, "kilimo cha mbogamboga kwenye vichuguu ni rahisi kumudu kwa sababu gharama yake ni ndogo na hakihitaji nguvu nyingi ya kumwagilia ama kuendesha zoezi hilo."

Aisha Choka ni mmoja wa majirani wa Mzee Seme amesema, amekuwa msaada mkubwa katika kuwapatia lishe ya matunda na mbogamboga zinazowasaidia kupata vitamin c kisha kupunguza udumavu wa akili.

Mkoa wa Songwe ni mmoja ya mikoa inayozalisha chakula kwa wingi, lakini inakabiliwa na udumavu kwa kiwango cha asilimia 42, ambapo kwa sasa mkoa umeanzisha kampeni ya lishe kwa watoto ikiwemo kuwapatia chakula cha mchana wanafunzi, na kuhakikisha shule zinalima mbogamboga na matunda Kwa ajili ya lishe kwa watoto hao.