Ahukumiwa miaka 30 jela kwa kumbaka mwanafunzi

Tuesday October 05 2021
jelapic
By Anthony Mayunga

Wambura Sukuru mkazi wa Mugumu leo Jumanne Oktoba 5, 2021 amehukumiwa  kifungo cha miaka 30 jela na kulipa faini ya Sh1 milioni na mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Serengeti  kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 13  na kumpa mimba.

Hata hivyo mwanafunzi huyo alifariki dunia baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji.

Hukumu katika kesi ya jinai namba 319/2020 imesomwa na Hakimu Mkazi, Adelina Mzalifu baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi watano upande wa jamhuri.

Advertisement