Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajali ya basi Serengeti yajeruhi watatu

Serengeti. Basi la Kampuni ya AM lililokuwa linatoka Mugumu Serengeti kwenda Mwanza limepata ajali katika Kijiji cha Bokore wilayani hapa na kujeruhi watu watatu.

Basi hilo lilikuwa na abiria zaidi ya kumi.

Polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo jana Alhamisi  alfajiri ya saa 12.35 na kwamba wanamshikilia dereva kwa mahojiano.

Mganga mkuu wa Hospitali teule ya wilaya, Emiliana Donald amethibitisha kumpokea majeruhi mmoja aliyemtaja kwa jina la Sosoni Philipo mkazi wa wilayani Serengeti.

Amesema majeruhi huyo alikuwa analalamika kupata maumivu sehemu ya mgongo na kuwa wanaendelea na tiba.

Hata hivyo, majeruhi wengine wametibiwa katika zahanati za watu binafsi na kuendelea na safari zao.