Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ajali yaua 18 Mkuranga, 15 wajeruhiwa

Muktasari:

Watu 18 wamefariki na wengine 15 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika kijiji cha Kilimahwewa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Dar es Salaam. Watu 18 wamefariki na wengine 15 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika kijiji cha Kilimahwewa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Aprili 15, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema ajali hiyo imehusisha lori na gari la abiria aina ya Toyota Coaster.

“Ni Kweli tuko kwenye eneo la tukio, ajali imetokea na imesababisha vifo vya watu 18 na majeruhi 15,” amesema Lyanga.

Amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi baada ya Coaster hiyo iliyokuwa ikitokea mikoa ya Kusini kwenda Dar es Salaam iligongana na lori hilo lililokuwa likitokea Kimanzichana.

Kamanda Lyanga amesema majeruhi katika ajali hiyo wamepelekwa katika kituo cha afya cha Kilimahewa.