Aliyebaka na kulawiti kwenye kaburi afungwa miaka 30 jela
Muktasari:
Hakimu Chiganga Ntengwa alitoa hukumu hiyo juzi baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali Mkoa wa Katavi, Jamila Mziray.
Sumbawanga. Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemhukumu Ally Rashid maarufu ‘Ally Mwizi’ kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka na kumlawiti mwanamke wa miaka 25 kwenye kaburi.
Hakimu Chiganga Ntengwa alitoa hukumu hiyo juzi baada ya mahakama kuridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali Mkoa wa Katavi, Jamila Mziray.
Hakimu Ntengwa alisema amemhukumu mshtakiwa huyo baada ya kumtia hatiani kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria Namba 154 ya adhabu sura namba 16.
Alisema hukumu hiyo itakuwa fundisho kwa mshtakiwa huyo ili akitoka gerezani awe na tabia njema kwenye jamii.