Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyehukumiwa kunyongwa, wakili anayemtetea asema hakuna maombolezo

Mshtakiwa Elia Kimela akielekea kupata gari la Polisi baada ya kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa na Mahakama kuu kanda ya Iringa iliyoketi Wilaya Mufindi. Picha na Mary Sanyiwa

Iringa. Mahakama Kuu Kanda ya Iringa iliyoketi wilayani Mufindi, imemhukumu  adhabu ya kunyongwa hadi kufa mkazi wa Kijiji cha Kisasa, Elia  Kimela (23) baada ya kukutwa na hatia ya kosa la  mauaji ya kukusudia dhidi ya  Alex Juma Mlembe (49) mkazi wa kijiji hicho.

Shauri hilo la mauaji namba  86/2021 ambalo lilikuwa na mashaidi watano kwa upande wa Jamhuri ambapo hukumu yake imetolewa Alhamisi Machi 30, 2023 katika Mahakama Kuu Kanda ya Iringa ambayo imeketi wilayani hapa.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Iringa iliyoketi wilaya hapa, Ilvin Mgeta amesema mahakama imeridhika na ushaidi ambao ulitolewa na mashahidi hao  kwa pande zote mbili wa mashtaka na utetezi  na kumtia hatini mshtakiwa Elia Kimela kwa kutenda kosa la mauaji.


Aidha Jaji huyo amesema mshtakiwa huyo ametiwa hatiani chini ya kifungu namba 196 cha kanuni ya adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho ya mwaka 2020 ambapo adhabu yake ni kunyongwa hadi kufa chini ya kifungu namba 197 cha kanuni ya adhabu.

Jaji huyo amesema kuwa Mahakama imeridhika bila kuacha shaka lolote mtuhumiwa aliyefikishwa katika Mahakama hiyo ndio aliyesababisha kifo hicho cha Alex Juma Mlembe.

Jaji huyo ameeleza maelekezo yaliyotolewa mahakamani hapa yalidai kuwa marehemu aliondoka nyumbani kwake Novemba 16, 2020 baada ya mshtakiwa kumpigia simu mke wa marehemu kwamba mkaa upo tayari ndio siku ambayo mume wake hakuonekana tena hadi ulipopatika mwili wake Novemba 22, 2020 akiwa amekufa.

"Katika ushahidi uliotelewa na mke wa marehemu Silyela Luvanda ni kwamba mshtakiwa alimpigia simu ili amwambie mume wake akanunue mkaa sababu yeye marehemu alikuwa anafanya biashara ya kuuza mkaa na mshtakiwa alikuwa ndio anamuuzia mkaa huo," amesema Jaji huyo.


Kwa upande wa mshtakiwa  alikiri kuwepo  katika kijiji cha Kisasa Novemba 16, 2020 ambapo katika utetezi wake alidai kuwa aliondoka Novemba 17, 2020 kwenda Makambako mkoani Njombe hivyo akadai utetezi huo hauwezi kuwasaidia chochote kwa sababu wakati anaondoka mauaji yalikuwa tayari yamefanyika.

Ilielezwa Mahakama hapo kuwa marehemu baada ya kwenda na pikipiki katika eneo ambalo mshtakiwa anafanya kazi yake ya kuchoma mkaa alimpiga na shoka kichwani na kisha kuondoka na pikipiki hiyo.

Baada ya tukio hilo Mshtakiwa alikamatwa Novemba 23, 2020 huko makambako na kufikishwa katika kituo cha Polisi Mafinga November 25, 2020  huku Novemba 26,2020 Mshtakiwa alienda kuonyesha mahali sehemu ambayo pikipiki alikuwa ameicha.

Kwa mujibu wa maelekezo ya mshtakiwa huyo, alisema aliitelekeza pikipiki hiyo katika mgahawa wa bibi Flora na kisha kukimbilia Makambako baada ya mshirika mwenza kutoppkea simu yake kwa ajili ya kutafuta mteja wa pikipiki hiyo.

Kwa upande wa shahidi upande wa mashtaka ulieleza mahakamani hapo kwamba wakati wanaenda kukamata pikipiki hiyo  katika Kijiji cha Maguvani wakiwa kwenye gari baada ya kukaribia mshtakiwa aliwaomba wasimamishe gari na kwenda hadi kwenye mgahawa huo  na kuchukua pikipiki hiyo ambapo Flora alimtambua mshtakiwa kuwa ndiye aliyeacha pikipiki hiyo.

Baada ya ushaidi huo Mahakama ilidai kuwa wana shida na ushaidi ambao umetolewa na mashahidi kwamba mshtakiwa aliwaongoza Polisi kwenda kukamata pikipiki. Inadaiwa kuwa ni ya marehemu pamoja na kuonyesha mahali ambako tukio hilo la mauaji lilifanyika.

Awali akizungumza kabla hukumu hiyo kutolewa   Mwendesha  Mashtaka wa Serikali Yahaya Misango amesema upande wa mashta hawana kumbukumbu zozote zinazoonyesha mshtakiwa amewahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai.

Hivyo Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kosa la mauaji ya kukusudia chini ya kifungu 196 cha kanuni ya adhabu  ambapo adhabu ya kosa hilo kinapatika katika kifungu namba 197 cha kanuni ya adhabu sura 16 ambayo ni kunyongwa hadi kufa hivyo kwa Msingi huo ni ombi kwa Mahakama  kuzingatia kifungu cha 197 cha kanuni ya adhabu katika kumpa adhabu mshtakiwa.


Pia upande wa Jamhuri uliiomba Mahakama chini ya kifungu 535 kifungu kidogo cha 3 cha sheria ya makosa ya jinai sura ya 20 kama ambavyo imefanyiwa marekebisho mwaka 2022 hukusu kielelezo P4 kwa upande wa mashtaka kuwa ilidhie kuwa mali  ambayo ilikamatwa katika kijiji cha Maguvani ilikuwa mali ya marehemu hivyo akabidhiwe Mke wa Marehemu ambapo Mahakama  ilidhia kukabidhiwa Pikipiki hiyo chini ya  kifungu hicho.

Kwa upande wa utetezi wa mshtakiwa ukiongozwa na Wakili Vedasto Chonya amesema kwa kuwa mtuhumiwa ametiwa hatiani kwa kosa la mauaji ukizingatia adhabu ya kosa hilo hakuna adhabu mbadala  zaidi ya adhabu iliyotolewa basi upande wa utetezi hatutakuwa na  maombolezo.