Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyekuwa Katibu Mkuu CCK kusomewa hoja za awali Mei 19

Muktasari:

  • Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inatarajia kuwasomea hoja za awali aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabi (53) na mfanyabiashara Yusuph Yusuph Mei 19, 2022.


Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inatarajia kuwasomea hoja za awali aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muabi (53) na mfanyabiashara Yusuph Yusuph Mei 19, 2022.

 Hatua hiyo ni baada ya upelelezi wa kesi hiyo ya kujifanya ofisa Usalama wa Taifa (TISS) kukamilika.

Uamuzi huo umetolewa leo Alhamisi April 28, 2022 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rhoda Ngimilanga wakati shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Awali, wakili wa Serikali Mwandamizi, Mwanaamina Kombakono ameieleza mahakama hiyo kuwa shauri hilo liliitwa kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Ngimilanga aliahirisha shauri hilo hadi Mei 19.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, wanadaiwa Desemba 24, 2021 katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), iliyopo wilaya ya Ilala, mshtakiwa Muabi kwa nia ovu, alijitambulisha kwa Nguling'wa Balghe kuwa yeye ni Ofisa Usalama wa Taifa, wakati akijua si kweli.

Shtaka la pili, Julai 10, 2021 katika ofisi hizo za BOT washitakiwa wote wawili, walijitambulisha kwa Clay Apio kuwa wao ni maofisa usalama wakati wakijua si kweli.