Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyeshiriki kuchanganya udongo wa Tanganyika, Zanzibar afariki

Muktasari:

  • Miongoni mwa walioshiriki tukio la kihistoria la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar katika sherehe za muungano Aprili 26, 2023 Khadija Abbas Rashid amefariki dunia

Zanzibar. Khadija Abbas Rashid (74) miongoni mwa walioshiriki kuchanganya udongo wa iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar amefariki dunia jana Jumanne Agosti 23, 2023 nyumbani kwake Rahaleo Mkoa wa Mjini Magharibi.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano ambapo wametoa taarifa hiyo katika mitandao yao mbalimbali ya kijamii.

Marehemu alihusika katika tukio hilo la mfano la kuchanganya mchanga Aprili 26, 1964.

Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Julius Nyerere na Zanzibar iliyokuwa ikiongozwa na Abeid Karume ziliungana na kuunda Tanzania.