Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyetapeli Sh600 milioni kwa uganga anaswa

Kamanda wa polisi wa mkoa Kilimanjaro , Ramadhan Mungi.

Muktasari:

Mtuhumiwa huyo alifanikiwa kutapeli fedha hizo baada ya mwanamke huyo kukataa ushauri wa awali kuwa ili dawa ya kufanya wanafunzi wafurike shuleni hapo ifanye kazi, waue mwanafunzi mmoja kimazingara. Alipokataa ushauri huo ndipo alipoambiwa atoe fedha ili atengenezewe dawa mbadala.

Moshi. Jeshi la Polisi limefanikiwa kumtia mbaroni mkazi mmoja wa jijini Dar es Salaam, anayetuhumiwa kujifanya mganga wa kienyeji na kumtapeli mke wa mmiliki wa shule moja ya sekondari Sh600 milioni.

Mtuhumiwa huyo alifanikiwa kutapeli fedha hizo baada ya mwanamke huyo kukataa ushauri wa awali kuwa ili dawa ya kufanya wanafunzi wafurike shuleni hapo ifanye kazi, waue mwanafunzi mmoja kimazingara. Alipokataa ushauri huo ndipo alipoambiwa atoe fedha ili atengenezewe dawa mbadala.

“Yuko hapo kituo kikuu cha Mkoa wa Kilimanjaro. Mimi nilimuuliza ilikuwaje akasema ni kweli alichukua fedha hizo lakini kwa makubaliano ya uganga. Inaonekana kuna zaidi ya uganga,” alidokeza polisi mmoja.

Kamanda wa polisi wa mkoa, Ramadhan Mungi aliomba apewe muda hadi leo atakapotoa taarifa sahihi, lakini wiki iliyopita aliyekuwa kaimu kamanda wa mkoa, Koka Moita alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo.