Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyetuhumiwa kumuua mama yake aachiwa huru

Muktasari:

  • Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro imemuachia huru mshtakiwa namba mbili katika kesi ya mauaji namba 4 ya mwaka 2022, Wendy Mrema (41) aliyekuwa akituhumiwa kumuua mama yake mzazi, Patricia Ibreck (66)


  

Moshi. Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro imemuachia huru mshtakiwa namba mbili katika kesi ya mauaji namba 4 ya mwaka 2022, Wendy Mrema (41) aliyekuwa akituhumiwa kumuua mama yake mzazi, Patricia Ibreck (66)

Mbali na Wendy, mshtakiwa mwingine aliyeachiwa huru ni mshtakiwa namba tatu, Waziri Ally (37), ambapo hatua hiyo imefikiwa baada ya upande wa mashitaka kuwasilisha ombi mahakamani la kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya washtakiwa hao.

Kesi hiyo ya mauaji namba 4 ya mwaka 2022, ilifika mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Januari 26, 2022 ikiwa na washtakiwa watatu ambapo mshtakiwa wa kwanza ni Omary Rang'ambo (32), Wendy Mrema ambaye ni mtoto wa Marehemu pamoja na  Waziri Ally.

Leo Ijumaa, Agusti 19, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Naomi Mwerinde, upande wa mashtaka umeeleza hauna nia ya kuendelea na shauri hilo dhidi ya mshtakiwa namba 2 na namba 3 na hivyo kuomba waachiwe huru.

Mahakama imeridhia maombi hayo na hivyo kuondoa shauri dhidi ya washtakiwa hao wawili,  na kuwaachia huru.

Hata hivyo, katika kesi hiyo ya mauaji namba 4 ya mwaka 2022 imebaki na mshtakiwa mmoja namba moja  ambaye ni Omary Rang'ambo ambapo itakuja tena Agosti 22, 2022 kwa ajili ya kutajwa.

Marehemu Patricia ambaye alikuwa ni muuguzi mstaafu wa hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi, alitoweka nyumbani kwake eneo  la Rau tangu Februari, 2021 hadi mwili wake ulipofukuliwa Januari 9, 2022 na mabaki yake kupatikana.