Asilimia 55 ya pombe zinazotumika nchini zinakadiriwa kuwa bandia

Muktasari:

Zaidi ya nusu ya pombe zinazouzwa nchini ni bandia zisizopita katika mifumo rasmi ya ubora na hazilipiwi kodi, imebainishwa.

Dar es Salaam. Zaidi ya nusu ya pombe zinazouzwa nchini zinakadiriwa kuwa bandia zisizopita katika mifumo rasmi ya ubora na hazilipiwi kodi, imebainishwa.  

Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jijini hapa, Mkurugenzi wa Tanzania Breweries Limited (TBL), Jose Moran alisema licha ya baadhi ya wazalishaji kufuata kanuni za ubora na kulipa kodi zinazotakiwa kisheria, soko la bidhaa zao linakabiliwa na ushindani wa pombe bandia sokoni.  
“Tanzania ina idadi kubwa ya watu wanaokunywa pombe feki. Inakadiriwa kuwa asilimia 54.7 wanatumia pombe hizo ambazo hazina ubora na hazilipiwi kodi,” alisema Moran.  
Licha ya mahitaji kuendelea kuongezeka, alisema gharama kubwa za uzalishaji viwandani zinasababisha bei yake iwe juu, jambo linalotumiwa na wanywaji wengi kuhamia kwenye pombe zinazouzwa kwa bei nafuu.  
Hata hivyo, alisema Serikali inapambana nazo kwa namna tofauti, ikiwamo kuanzisha matumizi ya stempu za kielektroniki.
“Risiti hizi zimesaidia kurasimisha lakini bei yake ni ghali,” alisema Moran.
Kupitia mfumo huo iliyoanzishwa Januari 2019, utaratibu wa kufuatilia na kujua kama bidhaa husika ni halisi au bandia umerahisishwa.
“Ikiwa upatikanaji wa kileo halali utawezeshwa, hiyo itaweka mazingira mazuri kwa wadhibiti kupata kodi kubwa kwa kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato,” alisema.
Hata hivyo, alisema kutokana na hali hiyo, Serikali imekuwa ikifanya juhudi za kudhibiti pombe feki ikiwa pamoja na kuanzisha matumizi ya stempu za kielektroniki (ETS).
“ETS zimesaidia kurasimisha lakini bei yake ni ghali,” alisema Moran.
Kupitia mfumo huo iliyoanzishwa na Serikali Januari 2019, kunakuwa na mfumo wa kufuatilia kama bidhaa husika ni halisi au feki na pia inazuia uingizwaji wa bidhaa zisizo na ubora sokoni.  
Akizungumza mchango wa kampuni hiyo kwa uchumi wa nchi, Moran alisema kwa miaka 10 mfululizo, kampuni hiyo imechangia kodi ya zaidi ya Sh3.7 trilioni.
“Ongezeko la thamani kwa uchumi kwa ujumla limekuwa Sh613 bilioni sawa asilimia 0.5 ya Pato la ndani la Taifa (GDP),” alisema  
Akizungumzia mchango wa kampuni hiyo kwa uchumi wa nchi, Moran alisema kwa miaka 10 mfululizo kampuni hiyo imelipa kodi ya zaidi ya Sh3.7 trilioni.
“Ongezeko la thamani kwa uchumi kwa ujumla limekuwa Sh613 bilioni sawa asilimia 0.5 ya pato la ndani la Taifa (GDP),” alisema.
Awali, Mkurugenzi wa Sheria wa kampuni hiyo, Mesiya Mwangoka alisema wanatumia zaidi mazao ya ndani kwenye malighafi wanazozitumia ili kuchangia kukuza uchumi.
“Asilimia 74 ya malighafi zinazotumika kutengenezea bidhaa zetu zinatoka ndani zenye thamani ya Sh130 bilioni, wakati kampuni ikitumia Sh1.755 trilioni kwa mwaka,” alisema.
Alisema katika kukuza upatikanaji wa malighafi, mwaka 2020 kampuni hiyo imeingia mkataba na Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) kusaidia mradi wa wakulima 2,000 wa mtama.
 “Mradi huo unawasaidia wakulima kupata mbegu, bima ya mazao, utunzaji wa shamba, utaalamu wa kilimo na kutoa mikataba ya masoko, hali iliyochangia kuongeza asilimia 70 ya uzalishaji wa mtama kuliko mwaka uliopita.
“Matokeo mazuri ya mradi huo yamewezesha kuongeza muda wa mradi mwaka 2021, ambapo wakulima wameongezeka na kufikia 4000,” alisema.