Askofu Maluma afariki dunia

Tuesday April 06 2021
kifopic
By Seif Jumanne

Njombe.  Askofu wa Jimbo Katoliki Njombe, Alfred Maluma amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Padri Justin Sapula wa jimbo hilo leo Jumanne Aprili 6, 2021 akieleza kuwa kimetokea usiku wa kuamkia leo saa 6:40 usiku katika hospitali hiyo.

Katika tangazo lake la kifo, Padri Sapula amesema taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika, “astarehe kwa amani baba mhashamu Alfred Leonhard Maluma.”Advertisement