Auawa kwa tuhuma wizi ‘kitimoto’

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa

Morogoro. Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Isack Ibrahimu (31) mkazi wa Bigwa manispaa hiyo, ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali baada ya kutuhumiwa kutaka kuiba nguruwe. Amesema mauaji hayo yametokea Februari 16 saa 9 usiku maeneo ya Bigwa baada ya mwenye nguruwe hao kumkuta kwenye banda na kuanza kumpiga huku akiita watu waliomshambulia hadi kifo.