Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aweso amsimamsha kazi meneja Ruwasa

Aweso amsimamsha kazi meneja Ruwasa

Muktasari:

  • Waziri wa Maji nchini Tanzania, Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Meneja wa Wakala wa Usambazaji wa Maji vijijini (Ruwasa), Mhandisi Nevard Kihaka kwa kumdanganya na kumpa taarifa za uongo juu ya upatikanaji wa maji katika vizimba 14 Kati ya 16 jambo ambalo sio kweli.

Rombo. Waziri wa Maji nchini Tanzania, Jumaa Aweso amemsimamisha kazi Meneja wa Wakala wa Usambazaji wa Maji vijijini (Ruwasa), Mhandisi Nevard Kihaka kwa kumdanganya na kumpa taarifa za uongo juu ya upatikanaji wa maji katika vizimba 14 Kati ya 16 jambo ambalo sio kweli.

Aweso amemsimamisha kazi jana Julai 13 wakati alipotembelea baadhi ya vilula hivyo vya maji kujiridhisha na kukuta maji hayatoki.

"Kwa kuwa umenidanganya na huku ndiko mnakofanya kazi na tunafanya kazi na wewe na ndiyo tumekuamini na sisi ndio tuliokuteua uje hapa  utusaidie na ukatudanganya wewe hapa hautufai. Mimi ninavyoondoka hapa leo chukua mabegi yako uondoke ,"amesema Waziri Aweso

Aidha alimpa siku moja Mhandisi aliyekuwa anasimamia Mradi wa Maji Shimbi na kuhamishwa Ileje arudi Rombo mara moja na akamtwe ili ajibu kwanini hakukamilisha Mradi huo pamoja na kujibu fedha za serikali alizipeleka wapi.

"Mhandisi aliyesimamia Mradi huu na kuhamishiwa Ileje arudi Alhamis hii na akamtwe na aeleze ni kwanini Mradi huu haujatekelezwa kama ilivyokusudiwa ilhali amechukua fedha za serikali," amesema.

"Hawezi kuharibu Rombo alafu akahamishiwa sehemu nyingine haiwezekani ,nataka Alhamis afike akiwa na mkandarasi wakamatwe na waeeleze kwanini walichukua fedha za serikali na wananchi hawana maji,mkuu wa Wilaya naomba usimamie hili," amesema Aweso

Awali Meneja huyo alimhakikishia Waziri Aweso kuwa vizimba 14 Kati ya 16 ndio vinatoa maji hali ambayo ilipelekea wananchi kuingilia Kati huku wakimweleza Waziri kuwa taarifa hizo sio za kweli ndipo Waziri alipotaka kwenda kuangalia baadhi ya vilula hivyo na kukuta havitoi maji.