Baba wa Michael Jackson afariki, alisema azikwe karibu na mtoto wake
Muktasari:
Joe Jackson, alikuwa amelezwa hospitali
Las vegas,Marekani. Baba wa aliyekuwa mwimbaji maarufu duniani Michael Jackson amefariki dunia akiwa na miaka 89 kwa ugonjwa wa Saratani ya kongosho.
Joe Jackson, ilibainika kufariki kwake baada ya mjukuu wake Taj Jackson kutumia mtandao wake wa Twitter Jumatano kutoa taarifa za msiba huo.
Joe Jackson, alikuwa amelezwa hospitali wiki hii , ni baba wa watoto 11 mkewe alifahamika kwa jina la Katherine Scruse.
Amekuwa akipambana na Saratani tangu alipopata Kiharusi mwaka wa 2015.
Awali familia ilikuwa imesema suluhisho halikuwa rahisi kwa sasa kwani saratani hiyo ilikuwa katika hatua za mwisho.
Mmoja wa watoto wake Jermaine Jackson akizungumza na waandishi alisema awali kabla ya kifo kuwa "baba yangu yuko katika hali dhaifu sana, hana muda mwingi" na kuongeza kwamba "familia inahitaji kuwa naye hospitalini siku hizi zake za mwisho".
Kabla ya kufariki Joe alitaka azikwe karibu na Michael; mwanawe aliyeaga miaka tisa iliyopita na alizikwa katika makaburi ya familia.
Joe alikuwa meneja wa kikundi cha Jackson 5 cha Michael na ndugu zake.
Kikundi hicho kilijulikana kwa muziki mzuri lakini baadaye kikajitenga na Michael alizindua kazi yake ya kibinafsi ambayo ilimfanya akajulikana kama mfalme wa muziki wa ‘pop’.