Baba, wanawe watatu wafariki ajali ya moto

Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu, Amani Madumba aliyefariki kwa ajali ya moto pamoja na mawawe katika Kijiji cha Malolo B, Kata ya Malolo, tarafa ya Mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Muktasari:

  • Baba na watoto wake watatu wa kiume wamefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwa wanaishi kuteketea kwa moto Kijiji cha Malolo B, Kata ya Malolo, tarafa ya Mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Kilosa. Baba na watoto wake watatu wa kiume wamefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwa wanaishi kuteketea kwa moto Kijiji cha Malolo B, Kata ya Malolo, tarafa ya Mikumi wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

 Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Alex Mkama, uchunguzi unaendelea kujua chanzo cha moto huo na kwamba timu yake imefika eneo la tukio kwaajili ya taratibu mbalimbali na baadaye atauhabarisha umma.

Akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi Digital, Mwenyekiti wa kitongoji cha Malolo B, Sufiani Ramadhani Ndagama, amesema alipata taarifa ya tukio hilo saa 7.04 usiku wa kuamkia Mei 05, baada ya kufuatwa nyumbani kwake na baadhi ya wanafamilia ya Marehemu huyo.

Ndagama amesema alipofika eneo la tukio, alikuta tayari majirani wameanza jitihada za kuuzima moto huo na hivyo kuungana nao, na walipofanikiwa kuuzima, waliingia ndani na kukuta miili ya watu wanne inayosadikiwa kuwa ni ya Madumba (60) na wanawe wanaokadiriliwa kuwa na miaka tisa, sita na mine ikiwa imeungua.

“Hapa kijijini, Marehemu hakuwa akiishi na mama aliyezaa naye hawa watoto, kila mmoja aliishi kwake, hata hivyo tulizoea kuona watoto wakishinda kwa mama yao na jioni wanarejea kulala kwa baba yao," amesema Mwenyekiti huyo wa Kitongoji cha Malolo B.

Ndagama ameongeza kusema: “Awali marehemu alikuwa na mke ambaye walibahatoika kuzaa naye na watoto hao sasa ni wakubwa na wanaojitegemea, hata hivyo mama huyo alifariki miaka ya nyuma. Sasa hao watoto wadogo waliofariki, ni wale ambao Madumba alizaa na mwanamke mwingine, ingawa kila mmoja aliishi kivyake.”

Mwenyekiti huyo ameendelea kusema: "Tangu wamekuwa na mahusiano na mke mdogo anayekadiriwa kuwa na miaka 40 hivi, sikuwahi kuusikia ugomvi mkubwa kabisa baina yao, labda ugomvi mdogo mdogo wa mke kuhitaji mahitaji kama chakula na mzee kushindwa kutimiza kutokana na hali ya kiuchumi," amesema Ndagama.

Kwa mujibu wa Ndagama, katika tukio hilo, walipata msaada mkubwa kutoka kwa askari wa mkoa jirani wa Iringa tangu usiku wa manane, ambao kimsingi wanapakana na eneo la tukio wakisubiri askari na daktari wa Mikumi  ambao waliwaarifu walikuwa njiani.

Ameongeza kuwa nyumba waliyokuwa wakiishi marehemu hao ni ya udongo, iliyokuwa imeezekwa kwa bati, na kwamba miili yote imeungua vibaya na walikuwa wakisubiri taratibu za kisheria ili baadaye miili hiyo iruhusiwe kuzikwa.

Naye jirani wa marehemu, Sebastian Sebastian; amesema wao walishtuka kusikia moto kwenye nyumba hiyo ndipo walipoamka na kutoka nje, na kuanza kuuzima moto uliokuwa umetanda nyumba yote.

Amesema wao kama majirani siku ya Jana walimuona marehemu akiwa katika hali yake ya kawaida