Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bakwata yatangaza Eid ya kuchinja Mei 27 Dar

Muktasari:

  • Eid El Adh’haa inasherehekewa kuadhimisha kilele cha Ibada ya Hijja, ambayo waumini huchinja wanyama kama ng'ombe au mbuzi na kugawa kitoweo hicho kwa wasiojiweza na jamaa zao.

Dar es Salaam. Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), limetangaza Sikukuu ya Eid El Adh’haa itakuwa Mei 27, 2026 na sherehe za kitaifa zitafanyika jijini Dar es Salaam.

Eid El Adh’haa, ni sikukuu ya pili katika Uislamu inayosherehekewa kukumbuka utayari wa Nabii Ibrahim kumtoa mwanawe Ismail kama dhabihu kwa amri ya Mungu.

Lakini, msingi wake ni kuadhimisha kilele cha Ibada ya Hijja, ambayo waumini huchinja wanyama kama ng'ombe au mbuzi na kugawa kitoweo hicho kwa wasiojiweza na jamaa zao.

Taarifa ya sikukuu hiyo, imetolewa leo Jumatatu Mei 18, 2026 na kutiwa saini na Katibu Mkuu wa baraza hilo, Sheikh Nuhu Mruma.

Baraza hilo, limeeleza sherehe za Eid El-Adh'ha kitaifa kwa mwaka huu, zitafanyika Mkoa wa Dar es Salaam na swala itaswaliwa katika Msikiti wa Mfalme Mohamed VI Bakwata makao makuu Kinondoni kuanzia saa 1.30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid.

“Kwa niaba ya Bakwata Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir anawatakia Waislamu na wananchi wote maandalizi mema ya sikukuu hiyo,” imeeleza sehemu ya taarifa ya baraza hilo.