Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Balozi Amina: Dk Salim alinishauri nigombee urais

Muktasari:

  • Balozi wa zamani Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, Amina Salum Ali amesimulia namna alivyoamua kuacha kazi hiyo na kisha kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM katika uchanguzi mkuu wa mwaka 2015.

Dar es Salaam. Balozi wa zamani Afrika kwenye Umoja wa Mataifa, Amina Salum Ali amesimulia namna alivyoamua kuacha kazi hiyo na kisha kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM katika uchanguzi mkuu wa mwaka 2015.

Katika uchaguzi huo, Balozi Amina alishika nafasi ya pili kwenye mbio hizo zilizomuwezesha Hayati Dk John Magufuli kukabidhiwa kijiti cha kupeperusha bendera kabla ya kushinda na kuingia Ikulu.

Balozi Amina ambaye kwa sasa ni Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar amesema akiwa Tanga wakati wa harakati hizo za kuomba ridhaa ya CCM, alipigiwa simu na bosi wake akimtaka achague upande mmoja pekee kati ya kazi au safari hiyo ya urais.

“Mwenyekiti wa OAU akaniambia amua mawili: Jitoe kwenye mbio za urais au ondoka OAU, ikabidi nimtafute, nimemtafuta usiku (Dk Salim) kaka kuna hali hii na hii,” amesema Balozi Amina leo Septemba 30, 2023 wakati wa uzinduzi wa tovuti ya hifadhi ya nyaraka za Dk Salim.

Tukio hilo limekutanisha viongozi mbalimbali mashuhuri wa kitaifa na kimataifa waliomtaja Dk Salim Ahmed Salim katika sura tofauti zitakazosaidia kuwa alama, mafunzo kwa kizazi kijacho.

Balozi Amia amefaafanua: “Akaniambia mambo mawili nayakumbuka, akasema heshima ya kiongozi haiwezi kuvunjwa, pili akaniambia wewe unawakilisha wanawake wengine Tanzania, keep it up (endelea na safari ya urais).”

“Nikamwambia mkuu wangu hapana, kwa sheria za OAU mimi sitoki. Nitaendelea mpaka mwisho (kwenye safari ya urais), kwa sababu Dk Salim alinipa moyo kwa sababu yeye alikuwa kioo cha umoja wa Afrika nikaamua kuendelea mpaka nilipofika.

 “Kwa hiyo mimi na wengine aliofanya nao kazi hakuwa mchoyo kumsogeza mtu au kumsifia kijana ili aweze kupiga hatua zaidi katika ndoto zake. Sio rahisi kwa viongozi wa Afrika kuwa hivyo, wengi tuna nyongo zetu, lakini yeye hakuwa na nyongo wala chuki wala hofu ya kunyang’anywa nafasi yake.”