Bashe atoa somo la kilimo cha alizaeti kwa wadau

Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la alizeti unaofanyika mkoani Singida, leo. Bashe alikuwa akielezea mkakati wa serikali kuhakikisha upatikanaji wa mbegu na uzalishaji wa mafuta tani 450,000 kwa mwaka ya alizeti. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Akizungumza na wadau wa uzalishaji wa mafuta mkoani Singida leo, Bashe amewataka kutumia mbinu bora za kilimo kuzalisha mbegu za kutosha kuzalisha mafuta.

Singida. "Je, ni kiasi gani cha alizeti kinahitajika kuzalisha Tani 450,000 za mafuta. Ni swali ambalo limeulizwa na kutolewa na majibu na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akieleza mkakati wa Serikali katika mkutano wa kampeni ya kitaifa wa kilimo cha alizeti unakofanyia mkoani hapa.

Mkutano huo ulilenga mikoa mitatu ya Singida, Dodoma na Simiyu kama mikoa ya kielelezo pia umejumuisha wadau wa kilimo kwa nchi nzima.

Katika majibu yake, Bashe amesema zaidi ya tani milioni 1.6 za alizeti zinahitajika kupata kiwango hicho cha mafuta ambayo ni mahitaji ya nchi kwa mwaka.

"Tija ya alizeti kwa ekari ni kilo 400 Hadi 800 ambayo ni sawa na Tani moja hadi tani 1.2 kwa hekta. Eneo linalohitajika kuzalisha tani zaidi ya milioni 1.6 ni hekta zaidi ya hekta milioni 1.6," amesema Bashe.

Bashe pia kwenye andiko lake ameweka swali lingine kamba ni kiasi gani cha mbegu bora zinazohitajika, akisema ili kuzalisha tani zaidi ya milioni 1.6 za alizeti, jumla ya tani 12,857  za mbegu bora zinahitajika endapo wakulima wote kwa asilimia 100 watatumia mbegu bora.

Amesema kwa kuwa kiwango cha matumizi ya mbegu bora za alizeti mchini ni asilimia 43, hii inafanya mahitaji halisi ya mbegu bora kuwa Tani 5,528, hivyo asilimia 57 onayobaki sawa na Tani 7,329 zinatokana na mfumo usio rasmi.

Amesema kutokana na uzalishaji wa Sasa ndani ya nchi wa tni 886 za mbegu bora za alizeti unafanya upungufu wa mbegu bora za alizeti kuwa Tani 4,662.

Pia ametaja changamoto wanazokabilian nazo wakulima ni huduma duni za ugani, upatikanji wa mbegu bora, bei kubwa ya mbegu za alizeti zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, mabadiliko ya tabia nchi, mtumizi hafifu ya embejeo za kilimo na uwepo wa visumbufu vya alizeti.