Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bashungwa ampa kazi kigogo wa Tarura

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa (aliyesimama) akizungumza katika kumbukizi ya miaka miwili ya kifo cha aliyekuwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT) na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Samson Mushemba ambaye alifariki Aprili 09, 2020.

Muktasari:

Bashungwa amemwagiza Meneja Tarura Manispaa ya Bukoba kufanya utafiti wa barabara yenye urefu wa mita 700 ili iweze kutengenezwa

Bukoba. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa amemwagiza Meneja Tarura Manispaa ya Bukoba, Adondile Mwakitalu kufanya utafiti wa barabara yenye urefu wa mita 700 na kupeleka taarifa ofisini kwake Dodoma ili iweze kufanyiwa matengenezo haraka.

Agizo hilo limekuja baada ya mwenyekiti wa taasisi ya Mushemba ijulikanayo kama Mushemba Foundation Josephat Mushemba kueleza   changamoto ya ubovu wa barabara itokayo Bukoba mjini kwenda shule ya msingi Mushemba yenye urefu wa mita 700.

Waziri Bashungwa ametoa rai hiyo Aprili 09,2022 katika kumbukizi ya miaka miwili ya kifo cha aliyekuwa mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) na aliyekuwa Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Samson Mushemba iliyofanyika katika shule ya msingi Mushemba iliyopo kata ya Ijuganyondo Manispaa ya Bukoba.

"Meneja wa Tarura Manispaa ya Bukoba nakuagiza siku ya Jumatatu fanya utafiti wa barabara hiyo na ulete taarifa ofisini kwangu Dodoma ili barabara hii iweze kuwekewa mipango ya ujenzi mara moja"Amesema Bashungwa.

Mwenyekiti wa taasisi ya Mushemba Josephat Mushemba amesema kuwa shule ya mchepuo wa Kiingereza ya Mshemba inao wanafunzi wapatao 417 wavulana 213 na wasichana 214, kwamba  wanafunzi 236 wanasoma bila malipo kutokana na kutoka katika kaya maskini.

Aidha Askofu wa (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na pwani Alex Malasusa amesema kuwa, kila alichofanya Askofu Mushemba katika uhai wake kiligusa maisha ya watu hivyo akawataka watu mbalimbali wanapokuwa bado hai wanaishi duniani kufanya vitu vinavyogusa maisha ya watu .

Aidha katika kumbukizi hiyo Waziri Bashungwa amezindua bweni ambalo litatumiwa na wanafunzi wapatao 60 ambalo limegharimu Sh160 milioni.