Benki ya TCB inaunga mkono juhudi za Rais Samia katika kuwawezesha wanawake

Muktasari:

Machi 19, 2021 Tanzania iliandika historia mpya kwa kupata Rais wa kwanza mwanamke Mama Samia Suluhu Hassan ambaye alichukua nafasi hiyo kufuatia kifo cha mtangulizi wake Hayati John Magufuli.

Machi 19, 2021 Tanzania iliandika historia mpya kwa kupata Rais wa kwanza mwanamke Mama Samia Suluhu Hassan ambaye alichukua nafasi hiyo kufuatia kifo cha mtangulizi wake Hayati John Magufuli.

Kuchukuwa nafasi hiyo ilikuwa ni muendelezo wa kuandika historia kwake na Taifa hili baada ya kutumikia nafasi ya Makamu wa Rais kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano ambapo hapo pia alikuwa mwanamke wa kwanza.

Tangu akiwa Makamu wa Rais, Mama Samia alikuwa mfano bora na kiongozi makini aliyeamini katika uwezo wa wanawake kufanya yale yanayofikiwa kuwa hawawezi kuyafanya.

Imani ya Rais Samia kwa wanawake iliendelea kujidhirisha mara baada ya `kuapishwa kuwa Rais wa sita wa Tanzania ambapo aliwapa nafasi katika ngazi mbalimbali za juu za uongozi Serikalini na kwenye utumishi wa umma.

Kutokana na hilo tumeshuhudia mabadiliko makubwa katika suala zima uwezeshaji wa wanawake hususani katika shughuli za kiuchumi ambapo kundi hilo limekuwa likijengewa uwezo kuhakikisha wanajikwamua kiuchumi.

Benki mbalimbali na taasisi nyingine za kifedha zimekuwa zikiwapa jicho la kipekee wanawake kwa kuanzishwa bidhaa na huduma zinazowasaidia kuwakwamua kiuchumi.

Tanzania Commercial Bank (TCB) ni miongoni mwa taasisi za kifedha ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za Rais Samia kuwawezesha wanawake.

TCB imekuwa ikiwawezesha wanawake kupitia bidhaa na huduma zake, kuwapa elimu ya masuala ya ujasiriamali na kutoa mikopo yenye riba nafuu.

Kupitia makongamano ya wanawake na biashara ambayo ni majukwaa maalumu ya kuchochea maendeleo yao binafsi, familia, jamii na Taifa kwa ujumla, Benki ya TCB imeweza kuwafikia wanawake wengi na kubadiliha maisha yao.

Makongamano hayo makubwa yanawakutanisha wanawake wafanyabiashara, wajasiliamali, waajiriwa, waliopo vyuoni wateja wa benki hiyo na wasio wateja kwa lengo la kumfanya mwananmke kujitambua kuwa yeye ana wajibu mkubwa katika kukuza uchumi wa Taifa.

Kwa kutambua mchango mkubwa wa mwanamke kuanzia ngazi ya familia TCB imedhamiria kuinua hadhi ya wanawake nchini kifedha kwa kuwawezesha kiuchumi na kuwasaidia kuwa wajasiriamali shupavu kupitia mikakati mbalimbali endelevu ikiwemo makongamano hayo.

Makongamano hayo yamefanyika katika mikoa ya Dodoma, Mwanza, Mbeya na visiwani Zanzibar ambapo wastani wa wajasiriamali 250 huwa wanaudhuria makongamano haya.

TCB inatekeleza jukumu hilo muhimu kwa kuwa kinara wa huduma jumuishi za kifedha za akinamama na kiongozi mbunifu wa huduma hizo sokoni.

TCB ni benki iliyojiandaa katika kuwawezesha wanawake kwa sababu Iko imara kifedha, ni hodari wa huduma za kidijitali na bingwa wa ubunifu ikiwa na wigo mpana wa huduma na mtandao mkubwa wa kuzifikisha popote kwa wakati.

Benki hiyo ina mtandao wa matawi makubwa 46, madogo 36, ofisi za wakala za Shirika la Posta Tanzania 120, ATM 84 ambazo zimeunganishwa na ATM 350 za mtandao wa Umoja Switch jambo ambalo linaongeza urahisi wa kuwafikia wanawake wengi na kusaidia kuwawezesha kupitia matawi na vituo vyake vya huduma vilivyosambaa kote Tanzania Bara na Visiwani.

Ndani ya waka mmoja chini ya uongozi wa Rais Samia, TCB imefanikiwa kufungua matawi mapya na yenye muonekano wa kisasa sehemu zifuatazo; Mbinga, USA River, Kigamboni, Bukoba, Mbagala na Mpanda. Matawi haya yameongeza upatikanaji wa huduma za kifedha na ufanisi wakati wa utoaji wa huduma hizo.

Pamoja na mafanikio mengine chini ya Rais Samia, TCB ilifanikiwa kukamilisha uunganishwaji na benki ya TIB Corporate na kufanikisha kubadilishwa kwa jina kutoka TPB Bank Plc na kuwa Tanzania Commercial Bank tarehe 14 Julai 2021.

Ubadilishwaji wa jina umewezesha benki kupanua wigo wa utowaji wake wa huduma na kuanza kuhudumia taasis na wateja wakubwa. Benki pia imepata fursa katika kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya taifa kama SGR ambapo benki inatoa huduma za kibenki kwa taasis zinasohusika na utekelezaji wa mradi huo.

Mbali na kuandaa makongamano hayo benki hiyo imekuwa ikitoa huduma mbalimbali ikiwemo mikopo ya vikundi, mteja wa biashara ya katikati, mteja mkubwa na kampuni.

Benki hiyo ina akaunti za vikundi, watu binafsi, za kampuni za vikundi ambayo operesheni yake ni bure na katika kuelekea siku ya jumatatu tarehe 18 tuna akaunti maalumu kabisa kwa ajili ya wanawake inayojulikana kama tabasamu imbayo ipo kwa ajili ya mtu mmoja au kwa vikundi na siku hiyo ya kongamano tutawafungulia akaunti kwa watakaokuwa tayari.

TCB pia imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali kama namna ya ukuzaji wa biashara pamoja na kutumia changamoto kama fursa na hii ni maalumu kwa wanawake ambao wakianzisha biashara inapokwama kidogo tu huamua kuachana nayo.

Kupitia juhudi hizi, TCB inatoa mchango mkubwa katika kubadilisha hadhi ya wanawake nchini kifedha na kiuchumi, jambo ambalo linasaidia kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu sita.