Bima ya afya yatua kwa wagonjwa wa ukoma
Muktasari:
Liana amesema lengo ni kuwalea na kuwahudumia wazee wasiojiweza hasa walioathiriwa na ugonjwa huo ambao hawakuwa wakipata hifadhi katika familia zao kutokana na kutengwa.
Tabora. Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Tabora, Sipora Liana amesema wanawake 23 na wanaume 32 ambao wana ulemavu wa ukoma wataanza kupata huduma ya Bima ya Afya ya Jamii baada ya kulipiwa na wafadhili.
Liana amesema lengo ni kuwalea na kuwahudumia wazee wasiojiweza hasa walioathiriwa na ugonjwa huo ambao hawakuwa wakipata hifadhi katika familia zao kutokana na kutengwa.
“Wafadhili hawa wanataka kuona wazee hao wanapata huduma bora za afya na wawe na afya iliyoimarika,” amesema Liana.
Wakizungumza baada ya kupatiwa kadi hizo za bima, wazee hao wamesema hawana hofu tena ya kukosa huduma za afya.