Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Biteko akemea migogoro iliyoota mizizi Msalala

Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko akizungumza wakati wa uzinduzi wa bank ya Exim tawi la Kahama leo Februari 25, 2025. Picha na Amina Mbwambo

Muktasari:

  • Mbunge wa Msalala, Iddi Kassim ametumia jukwaa hilo kuwaomba radhi watendaji wa halmashauri ya Msalala, wananchi pamoja na wanachama wote wa CCM wa jimbo hilo, na kwamba pale walipotofautiana ni kutokana na harakati za kuwaletea maendeleo wananchi.

Kahama. Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko, amewaasa wanachama na viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Msalala, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, kuungana na kuondoa migogoro iliyopo ndani ya chama hicho ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Naibu Waziri Mkuu Dk Biteko ameyasema hayo leo Februari 25, 2025, wakati akihutubia kwenye mkutano mkuu maalum wa CCM jimbo la Msalala, uliolenga kusoma ilani ya utekelezaji ya CCM ya 2020-2025, katika jimbo hilo.

Amewataka wanachama hao pamoja na wananchi kwa ujumla kutatua migogoro baina yao, kusameheana, kupendana na kushikamana kutumia vyema rasilimali zilizopo wilayani humo kwani ni wilaya ya kimkakati, yenye rasilimali nyingi  ambazo zikitumika ipasavyo zinaweza kukuza uchumi na kuwaondolea umasikini wananchi wake.

“Viongozi tunaweza kutofautiana hapa na pale kwa msimamo, kwa tafsiri, kwa namna tunavyoona mambo lakini tusifike mbali tukavuana nguo mbele za watu, tukaacha kazi yetu ya kuwaletea maendeleo wananchi” Alisema Dk Biteko

“Tusipotafsiri hali yetu ya kijografia kama wilaya ya Kahama tukaacha kuungana kwa pamoja kama wanaCCM tukashughulika na maendeleo ya watu, tukaanza kushughulikiana  wananchi watatushangaa huko wao wanataka maendeleo hawatakimigogoro,” amesisitiza

Naye mbunge wa Msalala, Iddi Kassim ametumia jukwaa hilo kuwaomba radhi watendaji wa halmashauri ya Msalala, wananchi pamoja na wanachama wote wa CCM wa jimbo hilo, na kwamba pale walipotofautiana ni kutokana na harakati za kuwaletea maendeleo wananchi.

“Niwaombe radhi watumishi wa serikali popote ambapo niliwagusa, kwani nilipomgusa mtu yeyote yule wa serikali sikua mimi ilikuwa ni hawa wajumbe ambao walinituma niwaletee maendeleo” Alisema Iddi