Biteko ataka Wizara yake iongezewe wataalamu

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila (kushoto) akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyotembelea mgodi wa madini ya Tanzanite Mirerani wilaya Simanjiro mkoa wa Manyara leo.Picha na Filbert Rweyemamu

Muktasari:

Biteko amesema kwa sasa Wizara hiyo ina wafanya tathmini ya madini 16 ambao hawatoshi kwa kazi kubwa iliyopo.

Arusha.Waziri wa Nishati, Dotto Biteko amesema serikali inaendelea kuongeza idadi ya wataalamu wa kufanya tathmini madini ili kurahisisha utendaji kazi wa Wizara hiyo.
Akizungumza leo Jumatatu Machi 15,2021 wakati wa ziara ya kamati ya Nishati na Madini kwenye migodi ya madini ya Tanzanite kuwa kada hiyo ina wathamini madini 16 kwa sasa na wapo ambao wapo kwenye mafunzo kwaajili ya kuziba pengo lililopo.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa kwenye chumba cha tathmini ya madini ya Tanzanite Mirerani kwenye Kituo cha Pamoja wakati wa ziara ya kamati hiyo wilaya ya Simanjiro mkoa mkoa wa Manyara leo. Picha na Filbert Rweyemamu


Baada ya kuwasili kwenye eneo la mgodi huo Kamati ikiongozwa na Mwenyekiti,Dunstan Kitandula walipewa maelezo ya shughuli zinazofanywa na  Kituo cha Pamoja cha Tanzanite -Magufuli.
Katika kituo wabunge walitaka kufahamu usahihi wa tathmini inayofanywa na wataalamu hao iwapo haupendelei au kumpunja mchimbaji na mfanyabiashara wa madini hayo.

"Utaratibu wa kufanya tathimini kwenye madini ya Tanzanite unafanyika kitaalamu na kwa uwazi pale anayefanyiwa tathmini anapokua hajaridhika tunawaleta watathimini kutoka sehemu nyingine nchini," amesema Biteko