Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bodaboda wasema wameacha taarifa nyumbani

Muktasari:

Wakati wafanyakazi katika sekta ya Umma na binafsi wakipumzika leo kupisha sensa ya watu na makazi, madereva bodaboda katika majijiji ya Dar es Salaam na Mwanza wanaendelea na shughuli ya usafirishaji wa abiria na mizigo huku wakisema wameacha vielelezo vyumbani.

Mwanza. Wakati wafanyakazi katika sekta ya umma na binafsi wakitumia siku ya leo kupumzika kupisha sensa ya watu na makazi, hali ni tofauti kwa madereva pikipiki maarufu kama bodaboda ambao wameonekana wakiendelea na shughuli zao kama kawaida.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi leo Agosti 23, 2022 katika maeneo mbalimbali ya jiji la Mwanza na jiji la Dar es Salaam umebaini kupungua kwa idadi ya daladala zinazofanya safari zake katika mitaa ya jiji hilo huku bodaboda zikitumiwa kama mwarobaini wa upungufu  wa huduma ya usafiri wa daladala.

Akizungumza leo na Mwananchi dereva bodaboda katika kituo cha Posta jijini Mwanza, Filbert Mafuru amesema ameondoka nyumbani kwake asubuhi akiwa hajaesabiwa huku akidai ameacha vielelezo kwa mke wake ili makarani watakapofika nyumbani kwake wapate taarifa za msingi kuhusu familia yake.

"Pia nimeacha namba yangu ya simu kama kuna jambo wanadhani hawataridhika na majibu watanipigia ili niwafafanulie kwa undani," amesema Mafuru

Dereva wa pikipiki katika kituo cha Nyanza jijini hapa, Samwel Kagege amesema ugumu wa maisha umemlazimu kutoka kwenda kutafuta fedha ili kukidhi mahitaji ya familia kwani bila kufanya hivyo familia haitapata mahitaji ya muhimu ikiwemo chakula.

Pia amesema ili kutokwamisha Sensa amemuagiza mkewe na wanafamilia wengine waliolala kwake kuwepo hadi pale maakarani wa Sensa watakapofika kwa ajili ya kuwahesabu.

"Sensa ni muhimu kwa sababu inaisaidia serikali kutambua hali ya maisha ya wananchi wake ndiyo maana nimeacha taarifa zangu za msingi kwa mke wangu mawakala wakifika wahudumiwe. Lengo la kufanya hivyo ni kutokwamisha juhudi za serikali kutoa huduma kwa wananchi wake," amesema Kagege

Kwa upande wake, dereva bodaboda katika kituo cha Mwanza Hoteli, Fahad Hussein amesema ametoka nyumbani Saa moja asubuhi akiwa ameshahesabiwa huku akitoa wito kwa madereva wengine kutotumia kisinguzio cha kutafuta fedha kukwamisha sensa hiyo.

Hata hivyo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Adam Malima ameonekana akipita katika maeneo mbalimbali ya jiji la Mwanza kufuatilia sensa hiyo inavyoendelea ikiwemo katika mtaa wa Mirongo na Capripoint jijini hapa.


Wakati huo, Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania Bara, Anne Makinda amesema pamoja na Sensa hiyo kuanza leo Agosti 23, 2022, inatarajiwa kufanyika kwa siku saba mfululizo kuanzia leo.

Jijini Dar es Salaam hali hiyo pia imedhirika baada ya madereva hao kuonekana vituoni kwao wakiendelea na kazi zao.

Alizungumza na Mwananchi, mwenyekiti wa kijiwe cha Shule kilichopo Kinyerezi Tabata, Cassim Ali Mohamedi amesema wasingeweza kusubiri nyumbani kuhesabiwa kutokana na kutotambua siku husika ya kufikiwa na makarani. 

“Katika kijiwe hiki tuko bodaboda 45 na kila mtu ana familia, asilimia 20 wameoa. Tulikubaliana kuendelea na kazi kwa wale tulioacha taarifa nyumbani, nashukuru wote tulijipanga,” amesema.