Burna Boy mwanamuziki pekee wa Afrika kwenye tuzo za Grammy

Wednesday November 25 2020
grammy pic

Mwanamuziki wa Nigeria, Damini Ebunoluwa Ogulu maarufu Burna Boy

By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Mwanamuziki wa Nigeria, Damini Ebunoluwa Ogulu maarufu Burna Boy amekuwa Mwafrika pekee kuchaguliwa kuwania tuzo za Grammy mwaka 2021.

Jana nchini Marekani ndio walitajwa washiriki wa tuzo hizo zenye historia ya aina yake ulimwenguni ambapo Burna Boy alitajwa kuwania kipengele cha albamu bora ya ulimwengu kupita albamu yake ya Twice As Tall iliyotoka Agosti 14, 2020.

Albamu hiyo inazungumzia kwa kiasi kikubwa maisha ya miaka ya nyuma ya Waafrika jinsi yanavyoweza kutumika kama hamasa kufanya mambo makubwa hivi sasa.

Hii ni mara ya pili kwa mwanamuziki huyo kutajwa kwenye tuzo za Grammy. Katika tuzo hizo za mwaka 2020 alitajwa lakini tuzo hiyo ilinyakuliwa na Angélique Kidjo kutoka Angola.

Wanamuziki waliochaguliwa kuwania tuzo nyingi zaidi mwaka 2021 ni Beyonce ambaye ametajwa katika vipengele tisa akifuatiwa na Taylor Swift vipengele sita sawa na Dua Lipa.


Advertisement
Advertisement