CCM Arusha yamkaribisha Lowassa nyumbani
Muktasari:
CCM Arusha yamkaribisha nyumbani Lowassa yadai alikuwa safarini sasa amerudi
Arusha. Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Arusha kimemkaribisha nyumbani Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na kusema alikuwa safarini amerudi nyumbani.
Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Machi 1, 2019 Katibu Mwenezi wa CCM mkoa Arusha, Shaban Mdoe amesema Lowassa amefanya uamuzi wa busara kurudi nyumbani.
"Alikuwa safarini amerudi nyumbani, Arusha tutampokea na tunaimani tutashirikiana nae kuhakikisha CCM inashida kwa asilimia 100 uchaguzi serikali za mitaa na pia mwaka 2020 " alisema
Lowassa alijiunga na Chadema mwaka 2015 na kugombea nafasi ya Urais ambapo mkoa wa Arusha ndio uliathirika zaidi na kuhama kwake CCM.
Miongoni mwa viongozi wa CCM waliohama na Lowassa alikuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa Arusha, Onesmo Ole Nangole, Katibu Mwenezi Mkoa, Isack Joseph,Mwenyekiti wa UVCCM mkoa Arusha, waliokuwa madiwani zaidi ya 30 na viongozi wengine kadhaa.