CCM yatoa vyeti vya heshima watumishi watatu Sengerema

Sunday October 03 2021
CCM pcc
By Daniel Makaka.

Sengerema. Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Sengerema Mkoa wa Mwanza, kimetoa vyeti vya heshima kwa watumishi watatu na makada wake kwa kusimamia vema  miradi ya maendeleo kwenye maeneo yao

Watumishi hao waliopewa vyeti ni pamoja na Mkuu wa shule ya sekondari ya Katunguru, Baraka Msimba, Mkuu wa shule sekondari ya Sengerema Zakaria Kahema pamoja na aliyekuwa meneja wa Mamlaka ya Maji Maji na Usafi wa Mazingira (Ruwasa) Wilaya ya Sengerema Cassian Wittike.

Akikabidhi vyeti hivyo leo Oktoba 3, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Sengerema, Marco Makoye amesema watumishi hao wamefanya kazi kwa weledi mkubwa.

Wakati mkuu wa shule ya sekondari Katunguru, akipewa cheti cha kusimamia nidhamu shule na kuongeza ufaulu, sambamba na kujenga vyumba viwili vya madarasa kupitia mfumo wa P4R, mkuu wa shule Sengerema Sekondari amepewa cheti cha usimamizi bora wa ujenzi wa nyumba ya walimu kusimamia nidhamu ya walimu na wanafunzi shule .

Naye Cassian Wittike aliyekuwa meneja wa Ruwasa wa wilaya Sengerema, amepewa cheti cha kusimamia na kukamisha miradi ya maji iliyokuwa imekwama kwa muda mrefu wilayani Sengerema na Halmashauri ya Buchosa ambapo maji yanapatika kwa asimilia 54.

Katika upande wa wanasiasa waliopewa vyeti hivyo ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Sengerema, Yanga Makaga ambaye amepewa cheti cha kujitoa kuisaidia CCM zaidi ya Sh10milioni zilizotumika kukamilisha ujenzi wa ofisi mpya ya chama hicho.

Advertisement
CCM pc

Pia yumo Mwenyekiti wa CCM wilayani humo, Marco Makoye aliyepewa cheti cha uongozi bora na kuhakisha ofisi ya CCM inakamilika na wanahamia.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Sengerema, George Kazungu amewataka watumishi hao kutoishia hapo bali wazidishe juhudi kazini.

Akitoa shukurani kwa nibaya wa wenzake mkuu wa shule ya Sekondari Katunguru, Baraka Msimba amesema nidhamu ya kusimamizi wa fedha ubunifu na kukamilisha miradi ya maendeleo kwa weridi ndiyo Siri ya mafanikio ya wao kufika hapa walipofika leo.

"Hatutarudi nyumba katika suala zima la kusimamia Mali za umma Ili ziwanufaishe Wananchi," asema Msimba.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Senyi Ngaga ameipongeza CCM kwa kutoa vyeti hivyo kulingana kazi zao wanazofanya zinazoonekana machoni kwa watu.

Advertisement