Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chadema yatuma salamu CCM

Wananchi waliojitokeza mkoani Kigoma katika uzinduzi wa Operasheni +255 Katiba Mpya ya Chadema

Muktasari:

  • Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Magharibi limetuma salamu kwa viongozi wote wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi za vitongoji, vijiji, kata hadi majimbo kujiandaa kupisha nafasi hizo katika uchaguzi mkuu ujao wa Serikali za Mitaa na ule uchaguzi mkuu 2025.

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Magharibi kimetuma salamu kwa viongozi wote wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ngazi za vitongoji, vijiji, kata hadi majimbo kujiandaa kupisha nafasi hizo katika uchaguzi mkuu ujao wa Serikali za Mitaa na ule uchaguzi mkuu 2025.

Wakili Gaston Garubindi, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Magharibi amesema viongozi wote wa CCM katika kanda hiyo inayohusisha Mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi zenye jumla ya vijiji 403, hawakuchaguliwa kwa njia ya haki kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 hivyo wajiandae kuondoka.

Wakili ametoa kauli hiyo leo Jumatano Mei 17, 2023 katika uwanja wa Mwanga Center mjini Kigoma wakati wa uzinduzi wa “Operesheni +255 Katiba Mpya’’ inayohamasisha Watanzania kudai Katiba Mpya.

 “Kanda hii tumejiandaa na bado tunajiandaa katika maeneo mengine. Tunaamini na tunaomba Mungu atujalie tumalize operation salama, malengo yatimie na iwe mwisho wa utawala wa CCM katika majimbo 25 yote ya kanda hiyo.

“Kanda yetu kwa sasa inaongozwa na watu ambao hawakupigiwa kura na wananchi, wapo waliopita bila kupingwa, utakutana na wenyeviti wa vijiji na vitongoji ambao hawakuchaguliwa na wananchi, sasa kanda ya magharibi hatuwezi tena kuongozwa na watu ambao hawakuchaguliwa na wananchi,” amesema Garubindi.”