Chadema yazidi kuwashukia kina Mdee

Wednesday November 25 2020
chademaaapic
By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika amesisitiza kuwa chama hicho hakikufanya uteuzi wa wanachama wao 19 ambao jana Jumanne Novemba 24, 2020 waliapishwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuwa wabunge wa viti maalum.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 25, 2020, Mnyika amesema chama hicho hakijateua wabunge hao wala kupeleka orodha ya majina Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kusisitiza kuwa kwa mujibu wa katiba ya Chadema mamlaka ya uteuzi wa majina ya wabunge hao yapo kwa kamati kuu ya chama hicho.

“Kamati kuu ya chama haijawahi kufanya kikao cha kuteua majina ya wabunge wa viti maalumu wakati wowote, pili katibu mkuu wa chama ambaye ndiye mwenye mamlaka ya mawasiliano na NEC..., sasa mimi sijawahi kuwasilisha orodha yoyote tume ya hayo majina ya wanaoitwa waliopendekezwa wabunge wa viti maalum, “ amesema Mnyika.

Endelea kufuatilia Mwananchi Digital kwa taarifa zaidi

Advertisement