Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chalamila azitaka halmashauri kusimamia miradi ya barabara

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akiwa ameambata na Kamati ya Siasa ya mkoa wakikagua miradi inayotelelezwa na Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (Tarura).

Muktasari:

  • Wasimamizi wa miradi hususan ujenzi wa barabara watakiwa kuisimamia ili inapojengwa izingatia mabadiliko ya tabianchi.

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameziagiza halmashauri kuhakikisha miradi ya ujenzi wa barabara inayojengwa inazingatia mabadiliko ya tabianchi ili zinaponyesha mvua kusitokee madhara.

Pia ameitaka Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (Tarura) mkoa huo kutopeleka fedha kwanza kwenye ukarabati wa miundombinu hiyo hususan vivuko hadi pale mvua zitakapopungua na kufanyika usanifu wa kina.

Hivi karibuni Mamalaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitangaza kuwepo kwa mvua za El nino ambazo katika mikoa 14 kuna uwezekano zikanyesha kwa asilimia 60 hadi Desemba.

Miongoni mwa mikoa hiyo ni Pwani, Dar es Salaam, Geita, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Shinyanga, Simiyu, Kagera, Morogoro, Mara, Kigoma na Mwanza.

Hata hivyo, mvua hizo zilizoanza kunyesha mwanzoni mwa Novemba, zimesababisha madhara maeneo mbalimbali ikiwemo uharibifu wa miundombinu, vifo na kuacha baadhi ya wananchi bila makazi.

Chalamila ametoa maelekezo hayo leo, Novemba 27, 2023 akiwa ameambatana na Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) walipofanya ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na Tarura.

"Kipindi hiki cha mvua kuna maeneo mengi miundombinu imeharibika, maeneo yenye shida ya vivuko Tarura subirini kwanza sitisheni kupeleka fedha, labda liwe eneo ambalo lina shida sana, tusubiri hadi mvua zitakapopungua ili ufanyike usanifu wa kina," amesema.

"Yapo maeneo tunaweza kupeleka fedha lakini kisifanyike kile kinachokusudiwa, kutokana na mazingira, pia nizielekeze halmashauri kusimamia miradi inayojengwa ikaakisi mabadiliko ya tabianchi," amesema Chalamila.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu amesema barabara nyingi zinajengwa vizuri, lakini changamoto Iko kwenye ukarabati pale zinapotokea mashimo zimekuwa hazirekebishwi kwa wakati.

Amesema jambo lolote zuri linahitaji uangalizi na kuwataka Tarura kuweka utaratibu wa kuzifanyia matengenezo kwa wakati.

"Tarura mmekuwa mkijenga barabara nzuri, kunapotokea mashimo basi zikarabitiwe kwa wakati, tumegundua barabara nyingi hazikarabatiwi kwa wakati,"amesema na Mtemvu.

Meneja wa Tarura Mkoa, Geofrey Mkinga amesema wana mtandao wa barabara urefu wa kilometa 5,059.05.

Amesema mtandao huo umegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni barabara za mlisho (feedder), mkusanyo (collector) na za jamii (Community).

"Kati ya hizo urefu wa kilometa 610.67 ni barabara za  lami/ zege, kilometa 1,642.90 ni barabara za changarawe na kilometa 2,805.48 ni barabara za udongo ambazo  ndizo zenye hali mbaya,"amesema Makinga.

Kuhusu madhara yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha, Mkinga amesema zaidi ya maeneo 83 yameathirika kutokana na mvua hizo katika wilaya zote na kwa Wilaya Ubungo maeneo yaliyoathirika ni 28, Temeke 10, Ilala 11, Kinondoni 19 na Kigamboni 14.

"Baada ya mvua hizi kuanza kunyesha yapo maeneo mengi yameathirika, yale maeneo ambayo hayapitiki hatua za dharura zimechukuliwa ikiwemo kujenga vivuko vya muda, lakini pia tumeshindilia mawe kwenye maeneo yaliyokatika,"amesema.