Chama cha Wafanyabiashara wa Ufaransa na Tanzania (FTCC) kinakuza uhusiano wa Ufaransa na Tanzania

Wednesday July 14 2021
ftccpic

S: Ndugu Darmois, ni lini Chama cha Wafanyabiashara wa Ufaransa na Tanzania (FTCC) kilianzishwa?

C.D.: “FTCC kilianzishwa Januari, 2020. Chini ya msukumo wa Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frédéric CLAVIER, wanachama watano waanzilishi wa kampuni kubwa za Ufaransa zinazofanya kazi Tanzania, ambazo ni AGS Group, Bolloré, ENGIE PowerCorner, Maurel & Prom, TotalEnergies na mimi mwenyewe Mwenyekiti, tulijishughulisha na uanzishwaji wa FTCC.”

S: Nini lilikuwa lengo kuu la uanzishwaji wa FTCC?

CD.: “Chama cha Wafanyabiashara wa Ufaransa na Tanzania kinatoa fursa ya mabadilishano na mitandao ya biashara baina ya kampuni za Tanzania na Ufaransa na kinakusudia kusaidia ukuaji wa biashara za nchi hizo kwa kusaidia na kuwezesha shughuli za biashara, uwekezaji, fedha na viwanda.

FTCC pia kinakuza na kuwezesha uanzishwaji wa ushirikiano kati ya kampuni za Ufaransa na Tanzania ili kuongeza nguvu zao kwenye soko la kimataifa. “Ufanyaji biashara pamoja” na “Ukuzaji uwekezaji Tanzania” umekuwapo tangu kuanzishwa kwa FTCC miongo miwili iliyopita.

Matukio ya ukutanaji wa wadau ana kwa ana, uendeshaji wa makongamano ya wavuti kwa mada mbalimbali zinazowakutanisha wataalamu kutoka sekta za umma na za binafsi chini pamoja na matukio mahsusi yanayohusisha wafanyakazi na wataalamu wa ufundi wa kampuni zetu yameandaliwa kwa kuzingatia miongozo hii.”

Advertisement

S: Je, Tanzania inaweza kufaidika moja kwa moja kutoka katika shu-ghuli za FTCC?

CD.: “Ni kweli, pia tumejitolea kuchangia kwa pamoja kuongeza juhudi za uwajibikaji wa kijamii. Kwa mfano, miezi michache tu baada ya kuanzishwa, FTCC iliratibu, kwa ushirikiano wa karibu na Balozi wa Ufaransa, msaada kutoka kwa wanachama wake vifaa vya kujikinga dhidi ya janga la Uviko 19 kwa wafanyakazi wa afya Tanzania. Kubadilishana mawazo na rasilimali, ambapo tunakuza na kuwezesha, tunalenga kujenga jamii yenye maadili na uwajibikaji zaidi.”

S: Je, unaiona wapi FTCC baada ya miaka ijayo?

CD.: “Ingawa bado ni taasisi changa, FTCC imekua zaidi mwaka huu kwa kupata wanachama wasiopungua 40 kutoka katika sekta za uchumi za Tanzania na Ufaransa. Tanzania inavutia na bado itaende-lea kuvutia wawekezaji na uwekez-aji huu ni muhimu kwa uhusiano wa kina na mkubwa wa kiuchumi, kiu-tamaduni na kijamii kati ya Ufaransa na Tanzania.

Tangu kuanzishwa kwake, FTCC imekuwa ikijitahidi kutekeleza jukumu lake la kukusanya sauti za wengi zisikike kwa kusimama katika nafasi inayoweza kutetea maslahi mapana ya wanachama wake.

Pia, tunazieleza wazi mamlaka kwa chambuzi zetu za pamoja kuhusu mitazamo au mahitaji ya sekta binafsi ili kujitahidi na kuchangia kwa ufanisi zaidi kwa maendeleo ya Taifa.” Mpaka kufikia mwisho wa Juni 2021, FTCC imekuwa mshiriki wa Mtandao wa Kimataifa wa vyama vya kibiashara vya Kifaransa katika nchi 124 duniani.

Hii inakusudia kuwapa wanachama wake fursa kubwa za kufungua masoko na uwekezaji duniani. Mafanikio haya yote yas-ingewezekana bila kuhusika kwa wanachama wa FTCC, washirika wa biashara na wanachama waanzilishi

Advertisement